Kikosi
cha Yanga kilicholambishwa shubiri na Simba, Uwanja wa Taifa Dar es
Salaam katika mechi ya "Nani Mtani Jembe" Desemba 2014
“Ni ndoto ya mchana Yanga kuwafunga mahasimu wao Simba”, Ndivyo unaweza kusema, itabaki kuwa historia kwani wapinzani wao wanajuwa mbinu za kuwafunga, wakati ushindi wa Yanga ni sare.
“Ni ndoto ya mchana Yanga kuwafunga mahasimu wao Simba”, Ndivyo unaweza kusema, itabaki kuwa historia kwani wapinzani wao wanajuwa mbinu za kuwafunga, wakati ushindi wa Yanga ni sare.
Kasumba iliyojengwa na viongozi wa Yanga kukimbilia kusajili kila mchezaji anayetakiwa na Simba itaendelea kuwafanya wafungwe kila watakapokutana, hali hiyo ikichagizwa pia na Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Mbrazil, Marcio Maximo.
Hivi karibuni Simba ilitangaza kumsajili mshambuliaji mkongwe wa Polisi Morogoro, Danny Mrwanda, baada ya Yanga kupata tetesi, viongozi wa klabu hiyo walifanya mipango ya haraka kumsajili kana kwamba wanawakomoa Simba, kumbe wanaongeza mamluki ndani ya klabu.
Hakuna asiyefahamu kuwa Mrwada ni mchezaji na mwanachama hai wa Simba, na uongozi wa Simba kutaka kumsajili ni mkakati mojawapo wa kumrejesha kundini kada huyo aliyekuwa akicheza soka la kulipwa nje ya Tanzania kwa muda mrefu.
Waswahili wanasema kikulacho ki nguoni mwako, kwa kiasi Fulani Simba imewekeza wachezaji wao ndani ya Yanga, wakati Yanga wenyewe hawajawekeza ndani ya Simba, kwa hali hiyo, Yanga isitegemee miujiza kuwafunga Simba.
Mtoto wa nyoka ni nyoka, Ndani ya Yanga wapo nyoka kama, makipa Ali Mstafa, Deogratius Munis na Juma Kaseja (anayeondolewa msimu huu, mlinzi kisiki Kelvin Yondan aliyesajiliwa Yanga mwaka jana na sasa wamemchukua kada mwingine mwandamizi wa klabu hiyo ya Msimbazi Danny Mrwanda na Amis Tambwe ambaye Simba wameona kiwango chake kimeshuka.
Kuhusu Kocha Maximo, ataendelea kuwaudhi mashabiki wa Yanga kwa kuwaleta wachezaji wenye uwezo mdogo ili wachezaji wenye wazawa wenye uwezo mkubwa wa kusakata soka wasipate namba. Kitendo cha Maximo kuwaleta ndugu zake Emerson Oliveira na Andrey Coutinho na kuwaacha Jerryson Tegete, Hussein Javu, Nizar Khalfan na Salim Telela wenye uwezo mkubwa ni kuiangamiza Yanga.
Wakati umefika Yanga watambue kuwa si kila Kocha kutoka Brazil ana uwezo, hebu tuwapatie kazi makoche wetu wazalendo, wenye mapenzi makubwa na Yanga kama Boniface Mkwasa, Fred Minziro na Juma Pondamali. Hakika Yanga itafanya vizuri, poleni wana Yanga wote.
Marcio Maximo
MCHEZO wa Nani Mtani Jembe, unaozikutanisha timu mbili kongwe zenye upinzani wa jadi nchini, Yanga na Simba imegeuka kuwa machinjio kwa makocha wa Yanga baada ya Kocha Mkuu, Marcio Maximo kutimuliwa rasmi jana.
Huu ni msimu wa pili mfululizo, kwa Yanga kuwafukuza makocha wake baada ya kufungwa na Simba, kwa kupoteza mchezo wa nani mtani jembe. Mchezo wa kwanza uliofanyika mwaka jana, 2013, Yanga ilifungwa 3-1 na kusababisha aliyekuwa kocha wake Ernie Brandts kutimuliwa pamoja na benchi lake la ufundi.
Mwaka huu Kocha Marcio Maximo nae amefungashiwa virago baada ya kungwa 2-0 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ukiwa mchezo wa nane wa ushindani baada ya michezo saba ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Maximo aliepokelewa na mashabiki wa Yanga kwa vifijo na nderemo Juni mwaka huu baada ya kutangazwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo, amewaaga rasmi wachezaji wakati wa mazoezi uwanja wa Sekondari ya Loyola Dar es Salaam jana.
Mazoezi hayo ya Jumanne asubuhi yaligeuka simanzi baada ya Maximo kuwakusanya wachezaji wake na kuwatakia maisha mema ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa walielezea kutoridhishwa na uamuzi wa uongozi wa kumuacha kocha wao na mshambuliaji Hamis Kiiza kutoka Uganda. Mmoja wa wachezaji hao alisema "Ni kweli kocha ametuaga!
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment