Imeelezwa kuwa sababu kubwa ya kurudiwa kwa uchaguzi wa Serikali za
Mitaa katika kijiji cha Bubale kata ya Masengwa wilaya ya Shinyanga
Vijijini uliokuwa unafanyika Desemba 14, 2014 na badala yake kufanyika
Desemba 16 ni kutokana na upepo wa ajabu uliobeba boksi la kura za
wagombea wakati zoezi la kupiga kura linaendelea.
Boksi la kura zilizopeperushwa na upepo ni lile la wagombea wa Uenyekiti wa kijiji cha Bubale.
Mashuhuda wakiwemo wasimamizi wa uchaguzi huo wamesema kuwa wakati zoezi la uchaguzi ghafla ulitokea upepo na kubeba boksi la kura kisha boksi hilo kujibamiza kwenye ukuta huku Mawakala wakijaribu kulizuia japo hawakufanikiwa na kura zikapeperushwa na upepo.
Kufuatia hali hiyo uchaguzi katika ngazi ya Uenyekiti uliahirishwa na kurudiwa jana, Jumanne huku mgombea kwa tiketi ya CCM, Bala Nundo aliibuka mshindi dhidi ya mgombea kwa tiketi ya CHADEMA.
Tukio la kura kupeperushwa na upepo limewaacha wakazi wa kijiji hicho midomo wazi huku wengine wakilihusisha na ushirikina.
- Kadama Malunde -Shinyanga: via Malunde1 blog: Maajabu,Sijui Uchawi!! UPEPO WA AJABU WAPEPERUSHA KURA ZA WAGOMBEA SHINYANGA VIJIJINI,UCHAGUZI WARUDIWA
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment