TATIZO hili huwakumba watu wengi kwenye jamii lakini kwa bahati mbaya wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadaye husababisha baadhi kuingia kwenye matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula.
Maumivu
chini ya kitovu hutokea kama ifuatavyo: Yapo yale ya chini ya kitovu
katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia
yapo ya aina mbili.
Kuna
yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita
mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo
mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande
zote mbili bila kusambaa kwa urefu.
Kuna
maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake wakati tu
wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu. Pia
yapo maumivu ambayo huwapata wanawake wakati wameinama, wakati wa
kunyanyua vitu vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine
wakiwa wamelala kifudifudi. Maumivu chini ya kitovu yanaashiria matatizo
gani kwa wanawake?
Mirija
ya uzazi kujaa maji mazito na machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye
mirija ya uzazi. Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na daktari kwamba
anatakiwa asafishwe kizazi chake/mirija ya uzazi na wakati huohuo
anasikia maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au upande mmoja kuna
uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana na kujaa
maji machafu.
Kutokukomaa
kwa mayai ya uzazi. Hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba
(ovaritis) na kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu mithili ya
kichomi.
Mwanamke
ambaye ana maumivu chini ya kitovu na wakati huohuo ana matatizo ya
hedhi, mfano hedhi kukoma au kutokuwa na mpangilio maalum kuna uwezekano
mkubwa akawa na tatizo la vifuko vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza
mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na kusababisha kuvimba
na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali mithili ya kichomi.
Kuvimba
kwa kuta za mji wa mimba na kuta za mirija ya uzazi (PID/Pelvic
Inflamatory Disease). Mwanamke anayesikia maumivu chini ya kitovu
katikati na pembeni kwa wakati mmoja na wakati huohuo akawa anatokwa na
uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi kuna uwezekano akawa na PID hasa
kama amewahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla
haijafikisha miezi mitano.
Afya
mbovu ya kibofu cha mkojo ikiambatana na matatizo ya maambukizi kwenye
mfumo mzima wa mkojo (UTI). Maumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya
mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana na mgonjwa kutoa haja ndogo kidogo
sana ila mara kwa mara.
posted by paparazi >>>
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment