WASHITAKIWA wanaokabiliwa na mashitaka ya kulawiti na kutuma picha katika mitandao ya kijamii, wamepandishwa kizimbani kusomewa maelezo ya awali ambapo walidaiwa kumlawiti mwanaume mwenzao na kumpiga picha kwa madai ya kutaka kulipwa Sh milioni moja.
Washitakiwa hao ni Erick Kasira (39) na Juma Richard (31) ambao wanadaiwa kulawiti sanjari na kupiga picha za tukio hilo.
Wakili
wa Serikali Mutalemwa Kishenyi alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi Said
Mkasiwa kwamba Agosti 23 mwaka huu, maeneo ya Maembe Bar & Guest
House, iliyopo Kiwalani Yombo walimkuta Kambi akiwa na Sanifa Bakari
katika chumba namba sita ambapo walimshutumu kuwa wana mahusiano baada
ya mshitakiwa mmoja kudai kwamba ni mke wake na kwamba wamemfumania.
Washitakiwa
hao walimtaka Kambi kutoa kila alichonacho na kuwakabidhi kompyuta aina
ya HP yenye thamani ya Sh 350,000, fedha taslimu Sh 100,000, simu aina
ya Tecno yenye thamani ya Sh 350,000 na viatu.
Walidaiwa
baada ya kumkuta Kambi akiwa na Sanifa kwa madai ya kwamba wana
mahusiano, walimlawiti kinyume na maumbile kisha walimpiga picha huku
wakiwa uchi.
posted by paparazi
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment