Friday, November 7, 2014

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
                                               
TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE) MWAKA 2014
1.0       UTANGULIZI
Katika Mkutano wake wa 102 uliofanyika tarehe 04/11/2014, Baraza la Mitihani la Tanzania liliidhinisha kutangazwa kwa matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ulifanyika kuanzia tarehe 10 hadi 11 Septemba, 2014.  Watahiniwa walifanya mtihani huo kwa kutumia Karatasi Maalum za Optical Mark Reader- OMR” ambazo zilisahihishwa kwa kutumia Mfumo wa kompyuta.  Matumizi ya teknolojia ya OMR kwenye Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi yalianza mwaka 2012.
2.0       USAJILI WA WATAHINIWA

Jumla watahiniwa  808,085 wa Shule za Msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 429,624 sawa na asilimia 53.17 na wavulana 378,461 sawa na asilimia 46.83.  Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 691 walikuwa ni wenye uono hafifu, watahiniwa 87 walikuwa ni wasioona, watahiniwa 374 wenye matatizo ya kusikia, watahiniwa 252 wenye mtindio wa ubongo na watahiniwa 27 wenye ulemavu zaidi ya mmoja.
Watahiniwa 792,122 sawa na asilimia 98.02 ya waliosajiliwa walifanya mtihani.  Kati yao wasichana walikuwa 422,625 sawa na asilimia 98.37 na wavulana walikuwa 369,497 sawa na asilimia 97.63.  Watahiniwa 15,963 sawa na asilimia 1.98  hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo utoro na ugonjwa.  Kati yao wasichana ni 6,999 sawa na asilimia 1.63 na wavulana ni 8,964 sawa na asilimia 2.37.
3.0       MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2014
3.1       Ufaulu kwa ujumla
Jumla ya watahiniwa 451,392  kati  ya  792,118 waliofanya mtihani huo  wamepata  alama  100  au zaidi katika alama 250. Idadi hii ni sawa na asilimia  56.99 . Kati yao wasichana ni 226,483   ambao ni sawa na asilimia 53.59 na wavulana ni 224,909   sawa na asilimia 60.87. Miongoni mwa watahiniwa waliofaulu wamo wenye ulemavu 795 (wasichana 355 ambao ni sawa  na asilimia 44.65 na wavulana 440 ambao ni sawa na asilimia 55.35 ya watahiniwa wote wenye ulemavu waliofanya mtihani). Mwaka 2013 asilimia ya watahiniwa walipata alama 100 au zaidi   ilikuwa 50.61, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 6.38.  
Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja mbalimbali umeainishwa katika jedwali lifuatalo:
Daraja
Wavulana
Wasichana
Jumla
Idadi
Asilimia
Idadi
Asilimia
Idadi
Asilimia
A
6,378
1.73
3,953
0.94
10,331
1.30
B
55,460
15.01
43,329
10.25
98,789
12.47
C
163,071
44.13
179,201
42.40
342,272
43.21
A-C
224,909
60.87
226,483
53.59
451,392
56.99
D
135,242
36.60
186,697
44.18
321,939
40.64
E
9,346
2.53
9,441
2.23
18,787
2.37
3.2       Ufaulu Kimasomo
Takwimu za matokeo zinaonesha kuwa ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 0.64 na 8.94 ikilinganishwa na mwaka 2013. Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambapo ufaulu ni asilimia 69.70 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Hisabati lenye ufaulu wa asilimia 37.56.  Mchanganuo  zaidi katika ufaulu wa masomo umeainishwa katika jedwali lifuatalo:
SUBJECT NAME
YEAR
CLEAN
PASSED (A-C)
GRADE D
GRADE E
KISWAHILI
2013
844,704
583,348
69.06
207,635
24.58
53,721
6.36
2014
791,924
552,003
69.70
198,993
25.13
40,928
5.17
KIINGEREZA
2013
844,678
300,001
35.52
437,695
51.82
106,982
12.67
2014
791,910
307,613
38.84
431,163
54.45
53,134
6.71
MAARIFA YA JAMII
2013
844,708
447,657
53.00
347,014
41.08
50,037
5.92
2014
791,938
454,043
57.33
296,592
37.45
41,303
5.22
HISABATI
2013
844,690
241,741
28.62
452,937
53.62
150,012
17.76
2014
791,869
297,411
37.56
387,489
48.93
106,969
13.51
SAYANSI
2013
844,570
401,059
47.49
378,834
44.86
64,677
7.66
2014
791,932
434,679
54.89
297,167
37.52
60,086
7.59
4.0       SHULE KUMI  ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI
Shule 10  bora Kitaifa katika PSLE  2014  zimeainishwa katika jedwali lifuatalo
NAMBA
JINA LA SHULE
IDADI
MKOA
NAFASI
PS0904095
TWIBHOKI    
33
MARA
1
PS1303065
MUGINI  
40
MWANZA
2
PS1307121
PEACELAND  
17
MWANZA
3
PS1304001
ALLIANCE  
25
MWANZA
4
PS1701035
KWEMA  
50
SHINYANGA
5
PS0501188
ST SEVERINE  
53
KAGERA
6
PS1701064
ROCKEN HILL   
58
SHINYANGA
7
PS0202083
TUSIIME  
168
DAR ES SALAAM
8
PS0702252
IMANI  
29
KILIMANJARO
9
PS1701062
PALIKAS  
19
SHINYANGA
10

5.0       WATAHINIWA WALIOPATA ALAMA ZA JUU KATIKA MASOMO
Wapo watahiniwa walioweza kufaulu kwa kupata alama 50/50 katika baadhi ya masomo ambapo English Language walikuwa 7,600, Kiswahili 32  na Hisabati 34. Ingawa  somo la Hisabati lina  ufaulu wa chini zaidi kuliko masomo yote, watahiniwa 34 wamepata alama 50/50  katika somo hilo ambapo kati yao Wasichana ni 08  na Wavualana ni 26  kama ilivyo  katika majedwali yafuatayo:
Orodha ya Wasichana waliopata alama 50/50  katika somo la Hisabati.
S/No
NAMBA  YA MTAIHINIWA
JINA LA MTAHINIWA
JINA LA SHULE
MKOA
1.         
PS0203012-166
RACHEL IBRAHIMU KIUNSI
KIMARA-'B'   
DAR ES SALAAM
2.         
PS0203077-020
MARIAM WILSON CHACHA
PARADIGMS   
DAR ES SALAAM
3.         
PS0401041-023
DIANA PETER NJAU
ST. CHARLES   
IRINGA
4.         
PS0501188-049
SOFIA GIDION NGERAGEZA
ST.  SEVERINE  
KAGERA
5.         
PS0904095-021
ANNABHOKE WAMBURA MAGORI
TWIBHOKI   
MARA
6.         
PS0904095-022
ATUGONZA NEWTON KAMZOLA
TWIBHOKI   
MARA
7.         
PS0904095-023
CATHERINE MOKORO MAGORI
TWIBHOKI   
MARA
8.         
PS1701035-041
EDINA NGASSA SHABU
KWEMA  
SHINYANGA
    
           
Orodha ya Wavulana  waliopata alama 50/50  katika  somo la Hisabati
S/No
NAMBA  YA MTAHINIWA
JINA LA MTAHINIWA
JINA LA SHULE
MKOA
1.         
PS0202109-010
OMEGA AMOS LUGATA
SABISA    
DAR ES SALAAM
2.         
PS0203058-021
JOHN REGINALD BUGERAHA
MOUNTEVEREST   
DAR ES SALAAM
3.         
PS0401043-026
MANSOOR MOHAMED MALAMBO
ST. DOMINICSAVIO    
IRINGA
4.         
PS0501188-007
ELIAH DANIEL MAKAMBA
ST.  SEVERINE  
KAGERA
5.         
PS0501188-013
GUSTAVIUS MWOMBEKI BAGAYA
ST.  SEVERINE  
KAGERA
6.         
PS0501188-017
MACHUMU NELSON SAMSON
ST.  SEVERINE  
KAGERA
7.         
PS0501188-018
MAPATO MAARIFA MAGESA
ST.  SEVERINE  
KAGERA
8.         
PS0501188-022
OBED LUCAS SAMWEL
ST.  SEVERINE  
KAGERA
9.         
PS0501188-023
OCTAVIUS IJUMBA MTAYOBA
ST.  SEVERINE  
KAGERA
10.      
PS0504092-004
DASTAN ADRIAN PIUS
OMUKALIRO   
KAGERA
11.      
PS0504092-009
DICKSON NOVATH NDAULA
OMUKALIRO   
KAGERA
12.      
PS0504092-015
MALICK AHMAD KUDABA
OMUKALIRO  
KAGERA
13.      
PS0504092-016
MATHIAS GODFREY LUGALABAMU
OMUKALIRO   
KAGERA
14.      
PS0504092-017
MICHAEL JONAS MICHAEL
OMUKALIRO    
KAGERA
15.      
PS0504113-021
ROBERT INNOCENT NOEL
TEGEMEO    
KAGERA
16.      
PS0702202-029
JUNIOR JOHNSON LOSARU
SCOLASTICA   
KILIMANJARO
17.      
PS0702202-042
SAMSON HEAVENLIGHT NKYA
SCOLASTICA   
KILIMANJARO
18.      
PS0904095-007
JAMES JOEL NYAROBI
TWIBHOKI    
MARA
19.      
PS0904095-017
ROLLY GEDI MABURA
TWIBHOKI    
MARA
20.      
PS0908004-020
EMMANUEL BENARD SARUNGI
BUHEMBA   
MARA
21.      
PS1101170-004
HAJI ADAM NJALAMOTO
ST.  MARY'S   
MOROGORO
22.      
PS1104004-004
ABDULKARIM MIRAJI SAIDI
UHURU    
MOROGORO
23.      
PS1701035-017
KISHIMBA MASUNGA SHIMBA
KWEMA    
SHINYANGA
24.      
PS1703005-032
JACKSON PHANUEL MANGAIDA
BUGARAMA    
SHINYANGA
25.      
PS2401020-013
MASANJA HEZIRON KABASA
IHULIKE    
GEITA
26.      
PS2405080-028
NTOBI PAULO SUMBUKA
KASANDALALA    
GEITA
6.0       MPANGILIO WA MIKOA NA WILAYA  KIUFAULU
(a) Mikoa Kumi iliyoongoza Kitaifa  ni 
MKOA
IDADI
WALIOFAULU 
   (A-C)
ASILIMIA
NAFASI
DAR ES SALAAM
59,576
46,434
77.94
1
KILIMANJARO
37,918
26,192
69.08
2
MWANZA
53,596
37,017
69.07
3
IRINGA
21,363
14,650
68.58
4
ARUSHA
34,348
23,250
67.69
5
TANGA
39,066
26,261
67.22
6
NJOMBE
17,115
11,389
66.54
7
KAGERA
37,306
24,501
65.68
8
GEITA
27,854
17,560
63.04
9
MTWARA
25,015
15,608
62.39
10
(b)  Wilaya  Kumi zilizoongoza Kitaifa  ni 
WILAYA
IDADI
WALIOFAULU        (A-C)
ASILIMIA
NAFASI
MPANDA MJI   (KATAVI)
1,345
1,207
89.74
1
BIHARAMULO   (KAGERA)
2,680
2,389
89.14
2
MOSHI(M)   (KILIMANJARO)
3,565
3,145
88.22
3
KIBAHA DC   (PWANI)
1,532
1,350
88.12
4
 ARUSHA (M) (ARUSHA)
9,097
7,919
87.05
5
KINONDONI(M)   (DAR ES SALAAM)
11,110
9,533
85.81
6
KOROGWE VIJIJINI   (TANGA)
4,868
4,118
84.59
7
ILALA(M)   (DAR ES SALAAM)
12,091
10,038
83.02
8
IRINGA(M)   (IRINGA)
3,250
2,681
82.49
9
MJI MAKAMBAKO   (NJOMBE)
2,179
1,785
81.92
10
7.0       WATAHINIWA WALIOFUTIWA MATOKEO
Baraza la Mitihani la Tanzania limefuta matokeo yote ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE), 2014 ya mtahiniwa 01 aliyebainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo. Idadi hii ni ndogo ikilinganishwa na watahiniwa 13 waliofutiwa matokeo yao mwaka 2013 kwa sababu za udanganyifu.
Baraza linachukua fursa hii kuzipongeza sana Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa, Wilaya na walimu wote waliosimamia mitihani hii kwa kuzingatia ipasavyo Kanuni za Usimamizi wa Mitihani ya Taifa. Aidha, Baraza linawapongeza kwa dhati watahiniwa wote waliofanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi, 2014 kwa kutojihusisha na udanganyifu katika mitihani.


8.0       HITIMISHO
Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi, 2014 yamewekwa  kwenye tovuti za Baraza  la Mitihani, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ili kila mtahiniwa aweze kuona matokeo yake. Tovuti hizo ni,
·        www.matokeo.necta.go.tz,
·        www.necta.go.tz au www.moe.go.tz
·        www.pmoralg.go.tz
Baraza la Mitihani la Tanzania   litawasilisha Matokeo hayo kwenye Mamlaka zinazohusika ili zifanye uchaguzi wa watahiniwa wa kujiunga na elimu ya Sekondari. Hivyo,  matokeo ya uchaguzi wa watahiniwa wa kujiunga  na Kidato cha Kwanza yatatangazwa na Mamlaka husika mara baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika.
Dkt. Charles E. Msonde
        KATIBU MTENDAJI

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!