Sunday, December 7, 2014


Mwigulu Nchemba akiwasili Uwanja wa MKutano Geita mjini.



 Kiongozi wa ACT Kanda ya Ziwa (Mratibu) akitoa shukurani zake za dhati kwa Mwigulu Nchemba kwa namna alivyokuwa mfano kwa kuwatetea masikini na wanyonge ndani na nje ya Bunge.

 Comrade Mwigulu Nchemba wakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita hiyo jana wakati wa mkutano.



"Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hatujazi nafasi, tunatafuta viongozi wenye uwezo wa kusimamia Halmashauri zetu za Vijiji, Mitaa na Vitongoji ili ziweze kufanya kazi za aendeleo kwa uadilifu na ufanisi wa hali ya kuridhisha"

Mwigulu Nchemba aliwasisitiza Wananchi kuchagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ndiyo wenye sera inayotekelezwa, hivyo wanajua mahitaji ya Wananchi wao.

"Kuna Wananchi wanatamani sana kubadilisha vyama kama nguo. Kubadilisha vyama siyo suluhisho la kutatua kero za maendeleo. Tujitahidi kufanya maamuzi yenye tija wakati wa uchaguzi, tuchague viongozi imara na wenye nia ya kuwaongoza. Achaneni na kubadilisha vyama vya siasa."

 Nchemba alisisitiza kuwa, 



"hakuna atakayeichafua Tanzania na abaki salama. Hakuna atakayeiba mali ya umma akatembea kifua mbele. Wahujumu uchumi wote wa nchi hii waanze kujiandaa kisaikolojia."


Mkutano ulimalizika na wananchi kuanza kurejea makwao.

Awali Mkutano huu ulipaswa Kurushwa Live na Star Tv, ila kwa bahati mbaya mitambo yao ilikwama. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

posted by wavuti.com

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!