Thursday, December 4, 2014

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC imekataa ombi la Mwendeska mashitaka mkuu, Fatou Bensouda, kuahirisha kesi dhidi rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. 


Bensouda amepewa wiki moja kutupilia mbali kesi hiyo au aiarifu Mahakama kwamba amepata ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi.

Uamuzi huo umekua unasubiriwa kwa hamu na gamu, baada ya rais wa Kenya kujielekeza Hague mwezi Oktoba. Kenyatta alitakiwa kuripoti mbele ya majaji wa Mahakama hiyo ili upande wa mashitaka na upande wa utetezi mbili waisikilizwe, na Mahakama iamuwe iwapo kesi hiyo iendelee au isitishwe.

Mahakama imechukua uamzi huo Jumatano Desemba 3. Awali Fatou Bensouda alikiri mwenyewe kwamba hana ushahidi wa kutosha, lakini aliomba apewe muda ili aendelee kutafuta ushahidi, akibaini kwamba mashahidi aliokua nao waliamua kujiondoa katika kesi hiyo. Bensouda aliituhumu serikali ya Kenya kwamba ilikataa kutoa ushirikiano.

Bensouda alikusudia kupata ushahidi kutoka upande wa serikali ya Kenya, akiitaka serikali kutoa nyaraka muhimu zinazo muhusu Kenyatta ambazo zingelionyesha kuwa alihusika katika ghazia za baada ya uchaguzi katika mwaka wa 2007 hadi 2008. Hata hivyo Mahakama ilitupilia mbali kwamba serikali ya Kenya ilikataa kutoa ushirikiano.

Rekodi zinasema kiasi cha watu 1200 waliuawa katika ghasia hizo.

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!