Saturday, November 8, 2014

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Mohamed amewasihi wanawake walioolewa kuwajibika katika masuala ya unyumba kama maandiko ya dini yanavyoelekeza.
Kamanda huyo alitoa wito huo baada ya kutakiwa kutoa taarifa ya kukatwakatwa na panga kwa mwanamke mmoja kutokana na kukataa kufanya tendo la ndoa na mumewe kwa sababu ya uchovu.


Kamanda Mohamed alisema alikuwa hajapata taarifa za kutokea tukio hilo, lakini akashauri wanawake walioolewa kuwajibika katika masuala ya unyumba ili kupunguza migogoro ya ndoa.

Mwanamke huyo mkazi wa Sigunga wilayani Uvinza, Jasmin Kassim alilazimika
kufanyiwa upasuaji kwenye Hospitali ya Misheni ya Heri wilayani Kasulu kuunga mifupa ya mikono yake baada ya kushambuliwa na mumewe.
Akisimulia mkasa huo juzi, Kassim alidai kuwa Oktoba 29 saa 4:00 usiku, baada ya kumaliza kula chakula alikwenda chumbani kulala ndipo mumewe alipotaka haki yake ya ndoa, lakini alimwambia kwamba alikuwa amechoka.

“Kilichonikuta baada ya kumkatalia alitoka nje na alirudi akiwa ameshika panga, ghafla akaanza kunipiga kisha kunikatakata katika mikono yote miwili. Nilipozinduka nikajikuta nipo zahanati ya kijiji, nikashonwa zaidi ya nyuzi tano,” alidai Kassim.

Kassim alisema kutokana na majeraha hayo alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Maweni iliyopo Ujiji ambako alilazwa. Baada ya uchunguzi iligundulika kuwa mifupa ya mikono imeachana na ndipo akafanyiwa upasuaji kwa mara ya pili.

  • Mwananchi: Kamanda: Wanawake wawajibike kwa waume zao

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!