Thursday, November 13, 2014

Mwanamke aliyefanyiwa upasuaji akiwa taabani 

Daktari anayehusishwa na tukio la vifo vya watu 13 katika kituo kilichokua kikitoa huduma ya kuzuia uzazi kwa njia ya upasuaji jimboni Chattisgarh nchini India,amekamatwa.


Dokta RK Gupta na msaidizi wake waliwafanyia upasuaji wananawake 83 katika kijiji cha Pendari.

Ripoti zinasema Daktari huyo aliwafanyia upasuaji wanawake 83 kwa saa tano, Serikali inasema Daktari mmoja anapaswa kutoa huduma ya upasuaji kwa Watu 35 kwa siku.

Wanawake wengine wawili walipoteza maisha baada ya kufanyiwa uapsuaji huo.

Zaidi ya wanawake 90 wako hospitalini wengi wao wakiwa katika hali mbaya,baada ya upasuaji.

Maandamano yamefanyika baada ya tukio la vifo , Serikali ya jimbo la Chhattisgarh imetoa amri ya kufanyika kwa uchunguzi,bado haijafahamika chanzo cha vifo hivyo.

Maafisa wa afya jimboni humo wamekana kuhusika na tukio hilo, lakini baadhi yao wamesema walikua katika hali ya kushinikizwa na mamlaka kufanya operesheni nyingi kwa muda mfupi.

POSTED BY BBC

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!