Mwanamke mmoja amejilipua katika chuo cha mafunzo Kaskazini mwa Nigeria.
Walioshuhudia
shambulizi hilo wanasema kuwa bomu lililipuka huku mwanamke huyo
akijiandaa kuingia katika ukumbi uliokuwa umejaa wanafunzi mjini
Kontagora.Idadi ya majeruhi bado haijulikani , lakini mwalimu mmoja alimbia BBC kuwa aliona miili minne ikiwa katika hali mbaya.
Wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram wanaendesha harakati za kivita dhidi ya serikali ya Nigeria, harakati ambazo zimekuwa zikiendelea kwa miaka mitano iliyopita.
Kundi la Boko Haram, limeyatangaza kuwa dola za kiisilamu baadhi ya majimbo wanayoyadhibiti, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. .
Kadhalika kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi na mauaji Kaskazini Mashariki mwa Nigeria tangu kuanzisha harakati zake mwaka 2009.
Watu wanasema walisikia mlio mikubwa kabla ya watu kuanza kukimbilia usalama wao.
Wanajeshi walikimbia kwa harakan katika kituo hicho baada ya shambulizi na hata kuziba eneo zima.
Tatu kati ya miili minne iliyoonekana ilikuwa ya wanawake.
Baadhi ya walioshuhudia shambulizi hilo walisema kuwa mwanamke aliyekuwa amejifunga mabomu hayo pia aliuawa.
Takriban watu 7 walijeruhiwa vibaya ingawa walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment