Mkufunzi wa timu ya Rostov, Igor
Gamula amesimamishwa kazi kwa kipindi cha wiki tano baada ya kupatikana
na hatia ya kutoa maoni ya kibaguzi, Shirikisho la soka nchini Urusi
limesema.
Gamula aliadhibiwa baada ya kueleza wanahabari kuwa klabu yake ina ''wachezaji wenye ngozi ya rangi nyeusi wa kutosha,tuna sita ya aina hiyo.''
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 54 ameomba radhi kwa kila mmoja wa wachezaji hao.
Hata hivyo,amesisitiza kuwa kusudi ya maongezi yake ilikuwa utani. Aliongezea, ''nina uhusiano mkubwa na wachezaji wote wenye ngozi nyeusi.Vyombo vya habari vya Uingereza havielewi utani wetu sisi Warusi.
Hata hivyo Waziri wa michezo Afrika Kusini,Fikile Mbalula na Rais wa Shirikisho la soka nchini humo Danny Jordaan wameliomba shirikisho la soka duniani FIFA kuangalia kwa ndani maoni ya Gamula.
''Nchi yoyote,inayotarajiwa kuwa mwenyeji wa maandalizi ya kombe la Dunia inafaa kuwa karimu kwa taifa na kabila lolote bila kubagua kwa misingi ya rangi ya ngozi yao na hasa Urusi.'' Jordaan alisema hayo akirejelea fainali za mwaka 2018.
''Kwa hiyo naamini kuwa yeye (Gamula) anafaa kupewa adhabu kali zaidi.Hii si mara ya kwanza mambo kama haya yamesemwa nchini Urusi.''
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment