Sunday, July 27, 2014

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, ametinga ghafla bandarini Dar es Salaam leo asubuhi baada ya wafanyabiashara kuanzisha tafrani ya kudai kucheleweshewa huduma.

 
Waziri Mkuya alipofika bandarini hapo alikwenda hadi Mapato Hause baada ya  mawakala kuona kuwa wanacheleweshewa kupata huduma muhimu ambapo waliamua kulalamika kwake.
Alipofika Mapato Hause, Waziri Mkuya alilalamikiwa kuwa mtandao mpya unaotumiwa unaojulikana kwa jina la TSS ni mbaya na unachelewesha kazi.  “Mtandao huu unalalamikiwa hata na TRA, unasababisha tunapoteza muda mrefu hapa Mapato House,” walisema baadhi ya wafanyabiashara kwa nyakati tofauti.
Wafanyabiashara hao walimuambia Waziri Mkuya kuwa ni vyema serikali ikaurudisha mtandao wa zamani unaojulikama kwa jina la Escudo ambao ulikuwa hauna matatizo kama hayo wanayoyashuhudia sasa.
Cha ajabu ni kwamba wakati waziri anawasili eneo hilo, Kamishna  wa Forodha aliyejulikana kwa jina la T. Masamaki alikuwa hayupo, hali iliyowashangaza mawakala wengi waliokuwa wamemzunguka waziri.

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!