Sunday, July 27, 2014

TIMBWILI la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani.



Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.
 
Mpishi wa futari auza ishu.
Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kusema:


 “Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.”
Picha za tukio.
Mapaparazi wetu bila kuzubaa nao walianza kuchukua picha za tukio  hatua kwa hatua. Wakati Timbwili likiendelea, Joseph alikuwa akipiga mayowe kumuomba mpwa wake huyo amsamehe ili wayamalize kimyakimya na kumsihi asisambaze habari hizo zikafika mpaka nyumbani kwa mke wake.

Mke atimka kinyemela.
Katika hali ya kushangza, wakati wawili hao wakiendelea kuangushana chumbani, mke huyo alipata upenyo na kuchoropoka, akatimua mbio kwa kuhofia kipigo na kukwepa kamera za OFM.

Mlinzi wa gesti.
Timbwili la wajomba hao lilitulizwa na mlinzi wa gesti hiyo (jina halikujulikana)  ambaye alitumia mabavu na kufanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka kitako.


Mjomba agoma kwenda polisi.

Baada ya kutulizwa, Kelvin aling’ang’ania waende polisi lakini mjomba mtu alikataa katakata akimbembeleza mpwa wake kwamba wayamalize na kuahidi kutorudia tena mchezo huo huku akisema mwanamke huyo alimuwekea mtego wa makusudi.
 
Chondechonde Kelvin.
Baadhi ya waungwana waliofika kushuhudia tukio hilo walimsihi Kelvin kumsikiliza mjomba ‘ake na kupokea fidia kidogo kwani kuyasongesha mbele mambo hayo ni aibu kwa familia yao na kumtia matatani mjomba huyo kwa mkewe.

Mjomba ajikomiti kimaandishi.
Kufuatia maombi ya watu, akiwemo mlinzi wa gesti hiyo, Kelvin alikubali kumsamehe mjomba wake ambaye naye ‘alijikomiti’ kimaandishi (kopi tunayo) kumlipa Kelvin fidia ya shilingi laki tano (500,000) na kuahidi kutorudia kummendea mke wake.
Katika barua hiyo aliyoaindika Joseph kwa mkono, alikiri kukutwa na mke wa Kelvin na kusema anatoa shilingi laki tatu (300,000) siku hiyo kisha kiasi kinachobaki atatoa siku inayofuata.

Mgoni ageuka na kwenda kufungua kesi.
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni zinadai kuwa, Joseph alikwenda kituo cha polisi (jina halijajulikana) kumfungulia kesi mpwa wake Kelvin na mkewe Emiliani akidai walipanga kumfanyia fumanizi.



Endelea kufuatilia hapa tutakuletea muendelezo wa tukio hili kwa kadri litakavyotufikia.
POSTED BY PAPARAZI

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!