Wednesday, May 14, 2014



Hivi karibuni mwanamke mmoja huko Nchini Nigeria aliuawa na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi baada ya kumtuhumu kuwa anaiba watoto wa shule na kuwapeleka kusikojulikana.

Mwanamke huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alianza kupigwa na baadaye wananchi hao wakamuua kwa kumchoma moto.

Inadaiwa kuwa mwanamke huyu alikutwa na watoto wawili wa kike ambao ni wanafunzi, akiongozana nao na ndipo wananchi walipompiga  na hatimaye kumchoma moto hadi kufa.

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!