MISHEMISHE za uchaguzi wa Simba Sc utakaofanyika juni 29 mwaka huu zinaendelea kushika kasi na sasa zoezi la kuchukua fomu linaendelea.
Jana maeneo ya Msimbazi Kariokoo, jijini Dar es saaalm, makao makuu ya klabu ya Simba, mwanachama wa muda mrefu na mmoja wa waanzilishi wa Kundi la Friends of Simba (F.O.S), Evans Aveva aliteka maeneo hayo baada ya kusindikizwa na wanaosadikika kuwa wanachama wa Simba kwenda kuchukua fomu ya kugombe urais.
Kwa tulioshuhudia idadi ya watu waliomsindikiza Aveva, hakika kama kuna mtu ana nia ya kugombea urais wa Simba anaweza kugwaya.
Watu hao wanaosadikika kuwa wanachama wa Simba sc walimlaki Aveva barabara ya Lumumba na kumsindikiza kwa maandamo wakipitia barabara ya Uhuru na baadaye Msimbazi, yalipo makao makuu ya klabu yao.
Msafara huo ulizuiliwa na wahusika wa makao makuu ya klabu na kumruhusu Aveva kuingia na mtu mmoja tu kwenda kuchukua fomu, Said Tully ambaye naye alichukua fomu ya kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji.
Baada ya kuchukua fomu hizo, kwa kifupi Aveva alisema mamia ya wanachama waliojitokeza wanadhihirisha nini wanakitaka kutoka kwake.
Ni ngumu kujua moja kwa moja kuwa mamia ya watu waliojitokeza ni wanachama hai wa Simba sc kwasababu hawakuonesha kadi zao na hata kama wangeonesha isingekuwa rahisi kujua kama wanazilipia.
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment