Thursday, May 8, 2014



Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress kinaongoza katika uchaguzi wa kihistoria uliofanyika Jumatano. 

Maafisa wa tume ya uchaguzi wanasema kuwa baada ya hesabu ya matokeo ya awali ya nusu ya kura zilizopigwa ANC imejizolea takriban asili mia 60 ya kura zilizohesabiwa .

Chama cha upinzani cha Democratic Alliance, kinashikilia nafasi ya pili na asilimia 24 ya kura ikiashiria ongezeko maradufu ya kura ikilinganishwa na uchaguzi uliotangulia.

Chama kipya kinachoongozwa na aliyekuwa kiongozi wa tawi la vijana katika ANC Julius Malema, kinashikilia nafasi ya tatu na asilimia 5 ya kura zilizopigwa.

posted by BBC >>>

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!