Wakuu wa serikali nchini Nigeria wamejitetea vikali kuhusiana na shutma
za kushindwa kukabiliana na wimbi la mashambulizi kutoka kwa kundi la
wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram huku wakisema kuwa wamo vitani.
Msemaji wa serikali Doyin Okupe, amekanusha kuwa jeshi la taifa hilo limezidiwa nguvu na waasi hao au utawala wa taifa umeshindwa.
Aidha msemaji huyo anasema kuwa jeshi lina kazi ya kujaribu kuwalinda raia na kupunguza maafa kwani litakaposhambulia waasi lazima maisha ya wananchi yalindwe.
Maelfu ya watu wanaaminika kuuawa katika msururu ya mashambulio katika siku za hivi karibuni katika mji wa Gamboru Ngala, walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji wenye silaha walishambulia umati katika masoko na nyumba za watu.
Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekahu alikiri kuwateka nyara wasichana hao wengi wao walio kati ya umri wa miaka 16 na 18 na kusema kuwa atawauza kwani hawakupaswa kuwa shuleni toka mwanzo na kwamba badala yake wanapaswa kuolewa.
Wasichana wengine 11 walitekwa nyara Jumapili baada ya vijiji viwili kushambuliwa karibu na maficho ya wapiganaji hao.
Utekaji nyara wa wasichana hao umesababisha serikali ya Nigeria kulaumiwa na kukosolewa kwa kujikokota katika hatua zake dhidi ya wapiganaji hao.
posted by BBC >>>

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment