Thursday, May 8, 2014

Shirika la kimataifa la Amnesty International limetuhumu pande zote mbili zinazozozana katika mgogoro wa kisiasa nchini Sudan Kusini kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu na matendo mengine mabaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Shirika hilo linasema kuwa ushahidi wake umetokana na waathiriwa wenyewe kusimulia yaliyoawakumba baada ya kushambuliwa kwa misingi ya ukabila huku wakitendewa dhuluma za kingono.

Ushahidi wa visa vya ubakaji, wizi na uchomaji wa miji na vijiji pia umeripotiwa.
Kwa mujibu wa shirika hilo, maelfu ya watu wameuawa wengi wakiwa katika nyumba zao au katika maeneo ya kuhifadhi wakimbizi.

Kulingana na taarifa za kina zilizokusanywa moja kwa moja kutoka kwa waathiriwa na mashahidi, Ripoti hiyo inasema kuwa maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wameuwawa huku nyingi ya mashambulio yakichochewa kikabila.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wanapangiwa kukutana kwa mazungumzo ya amani hapo kesho ijumaa.
Umoja wa mataifa unatarajiwa hii leo kuchapisha ripoti yake ya ukiukaji wa haki za kibinadamu.

posted by BBC >>>

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!