Thursday, December 18, 2014

Waziri Ghasia 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia, amesema leo Jumatano Desemba 17, 2014, kuwa hatajiuzulu ng’o kutoka wadhifa wake kwa sababu ya kashfa ya kuvurugika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini Jumapili iliyopita.

Badala yake, waziri Ghasia amesema Wakurugenzi sita wa Halmashauri wamefutwa kazi, watano kusimamishwa huku wengine kushushwa vyeo baada ya kubainika kuwa walichangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, Desemba 2014.


Akitangaza hatua hiyo inayotokana na ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Ghasia amesema uamuzi huo umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.


Amewataja Wakurugenzi waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni wa Halmashauri za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda. Waliosimamishwa kazi ni Wakurugenzi wa Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na Manispaa ya Sumbawanga.


Watatu waliopewa onyo kali ni wa Rombo, Busega na Muheza. Wengine watatu waliopewa onyo la kawaida ni Wakurugenzi hao wa Manispaa za Ilala, Hai na Mvomero.


Soma zaidi vipande vifuatavyo vya taarifa hiyo...



 

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!