Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova alisema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema watuhumiwa hao wamehusishwa na vitendo hivyo baada ya upelelezi wa kina na wa kitaalamu uliosaidia kuwakamata wahalifu hao wakiwa na vielelezo mbalimbali.
Kova aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Abubakari Amani (28) Mkazi wa Mwenge na Ezekiel Kasenegala (25) mkazi wa Tandika, Dar es Salaam.
Pia alisema watuhumiwa hao walikiri kuhusika na mauaji ya Wenze Makongoro (23), aliyekuwa mwanafunzi wa Stashahada ya Ukutubi katika Chuo cha Bagamoyo na Jackline Frederic (30) mkazi wa kisarawe.
''Watu hao waligundulika kuuawa Novemba 19 Mwaka huu na kutupwa maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam,'' Alisema Kova.
Aliongeza kuwa baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao walikutwa na vielelezo mbalimbali ikiwamo suruali mbili za kike, sketi moja, kikoi kimoja, mikoba minne ya kike, simu moja aina ya tecno.
Pia sidiria moja, vidani vya mikononi viwili, pete moja, hereni jozi tatu, vibanio vya nywele, make -up tatu za kike na shanga tatu.
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment