MABOMU manane ya kutupwa kwa mkono ambayo yanasadikiwa kufukiwa chini
kwa zaidi ya miaka 10 yameokotwa kwenye kijiji cha Mabamba wilaya ya
Kibondo mkoani Kigoma.
Mabomu hayo yamegunduliwa na mafundi uashi wawili waliokuwa wakichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mganga wa kituo cha Afya Mabamba katika nyumba ambayo awali ilikuwa ikimilikiwa na diwani wa kata hiyo, Ally Amin Gwanko.
Fortunatus Katabalo Mmoja wa mafundi hao waliokukwa wakichimba na kusogeza kifusi cha udongo katika eneo hilo la ujenzi alisema kuwa waligundua kuwepo kwa mabomu hayo baada ya kuanza kuchimba na kukutana na kitu kinachofanana na chuma ndipo walipomwita msimamizi wa kazi hiyo kuona nini kilichopo na kubaini kuwa walichokuwa wakichimba kinaweza kuwa mabomu na ndipo walipoacha kuendelea kuchimba na kutoa taarifa polisi na jeshi la wananchi ambao walifika na kuyathibitisha.

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment