Watu kumi na watatu wamekamatwa
kufuatia sakata ya biashara haramu ya binadamu ambapo nusura mwanamke
mjamzito kuhadaiwa kutoa mimba yake kufuatia mpango wa kumuoza kwa
lazima kutibuka.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 20 kutoka Slovakia, aliuzwa kwa kima cha pauni, 15,000 na genge la wahalifu katika mtaa wa Great Macheseter.
Genge hilo lilimpangia mwakamke huyo kuolewa na mwanamume mmoja aliyekuwa anasubiri kutimuliwa kutoka nchini Uingereza kwa kuwa nchini humo kinyume na sheria.
Maafisa wa polisi walipokea taarifa kutoka kwa mwanamke huyo pale alipomwambia mkalimani kuwa aliozwa kinyume na matakwa yake na kwamba alichukizwa sana na pandekezo kuwa atoe mimba yake.
Wanaume kumi na wanawake watatu walikamatwa kufuatia kashfa hiyo.
Wahalifu hao walikuwa kati ya umri wa miaka 24 na 57 na walikamatwa kwa tuhuma za kushiriki biashara haramu ya kuwauza watu pamoja na kuwa na njama ya kuvunja sheria za uhamiaji.
Mnamo mwezi Mei, mwanamke huyo aliyekuwa na ujauzito wa wiki 25 alipelekwa katika mtaa wa Luton akidhani alikuwa anakwenda kuwatembelea jamaa wake.
Hapo ndipo alikutana na mwanamume mmoja aliyedai kuwa rafiki ya dadake na ambaye alimpeleka kwa mwanamume mmoja ambapo walimuoza kwa lazima mnamo mwezi Julai chini ya sheria ya kiisilamu katika mtaa wa Rochdale.
Baadaye mwanamke huyo alipelekwa hospitalini na rafiki mmoja wa dadake ambaye aliambia maafisa wa hospitali kuwa alitaka kutolewa mimba.
Polisi waligundua kuwa mwanamke huyo kwanza aliolewa kwa lazima na pili kukawa na mpango wa kumtoa mimba yake kwa lazima.
Polisi wanasema kuwa kuna visa vingi vya wanawake kuozwa kwa lazima na kuuzwa kama bidhaa nchini Uingereza.
POSTED BY BBC
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment