Mgeni
rasmi Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid akizungumza wakati wa kuzindua
kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo
katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya
kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Tatizo la ukosefu wa dawa katika hospitali kadhaa nchini, limekuzwa mno kuliko hali halisi na serikali itatoa taarifa rasmi kesho kuelezea tatizo hilo na hatua ambazo imechukua.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Rashid Seif wakati akijibu hoja za waandishi wa habari baada ya kufungua Kongamano la Wanahabari na NHIF mjini hapa.
Dk Seif alisema deni lililopo kwa sasa asilimia 80 ni kulipia gharama za dawa zilizoletwa kama msaada, lakini ununuzi wa dawa ni asilimia 20 pekee. Dawa hizo ni kama za UKIMWI, kifua kikuu na dawa za malaria.
Alisema kusema hali ni mbaya ni kulinganisha na lipi na dawa za aina gani na kusema zipo njia tatu za kupata dawa ambazo zimewezesha halmashauri kama Iramba kuwa na dawa wakati wowote.
Alisema vyombo vya habari vimekuwa vinakuza tatizo hilo ambalo kimsingi si kubwa hivyo.
Alisema hata hivyo kuwa ni kweli MSD inaidai serikali na ni kweli kuwa kuna shida ya madaktari, lakini tatizo la dawa sivyo lilivyo.
Alihoji kwamba, kama Iramba hawana tatizo la dawa kwa nini kwingine kuwa na tatizo la dawa kama MSD ni ile ile moja?
Awali akifungua kongamano hilo, aliwataka waandishi wa habari kuwa jicho la tatu la sekta ya afya ili kubainisha changamoto za huduma za afya katika maeneo mbalimbali ambako wanachama wa NHIF na Watanzania kwa ujumla wanapata huduma hizo.
Aidha aliwataka waandishi wa habari kutumia vyema kongamano hilo kujijenga na kuelewa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa lengo la kuhabarisha wananchi ili waelewe.
"Mojawapo ya mambo ya kuzungumzia ni ule mradi wa UDom ambao ukikamilika utakuwa umechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za matibabu nchini kwa maana ya vipimo vya kisasa na matibabu ya hali ya juu kabisa, na kuipunguzia Serikali gharama za kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu," alisema na kuongeza kuwa wananchi wanastahili kujua kinachofanywa na
wadau wa afya wakishirikiana na serikali.

- Lukwangule: Waziri ang'aka asema suala la dawa limekuzwa
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment