HALI si swari tena ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Hivyo ndivyo inavyoweza kutafsiriwa kutokana na joto linalolikumba Bunge hilo kutokana na hoja tata ambazo sasa wabunge wameshikilia bango wakitaka Bunge kujitokeza na kuonesha meno yake katika kuisimamia serikali kwa mujibu wa kanuni ya 63 (2).
Masuala yaliyosimamiwa na wabunge leo ni suala la fedha za akaunti ya Escrow Tegeta, mauaji ya kutisha wilayani Kiteto mkoani Manyara na uwajibikaji wa serikali katika siku za hivi karibuni.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM) ndiye alikuwa wa kwanza kuomba Mwongozo wa Spika, akishinikiza Bunge likubali kuunda Kamati Teule ili kuchunguza na kujadili madai ya ufisadi unaodaiwa kufanywa kwenye akaunti ya Escrow akidai kuwa kuna njama kwa ripoti hiyo kutowasilishwa bungeni.
Serukamba alisema suala la IPTL ni suala kubwa na sasa limesababisha wahisani kugoma kutoa fedha za kusaidia utekelezaji wa bajeti, lakini serikali imekuwa ikipiga danadana kuwasilisha ripoti kuhusu kuwepo kwa ufisadi katika Akaunti ya Escrow Tegeta.
Mbunge aliyefuatia kwa suala hilo alikuwa ni Mbunge wa Mkanyageni, Habibu Mohammed Mnyaa (CUF) aliyesema serikali sasa imeingilia mamlaka huru ya Bunge na hivyo ni lazima Bunge likatae hali hiyo.
Naye Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (CHADEMA) alilitaka Bunge kujadili tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu mauaji ya Kiteto, akisema serikali imeshindwa kulipatia suala hilo ufumbuzi.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Bunge Zungu aliposikiliza hoja hizo za wabunge alisema ni hoja nzito na zimefikia pabaya na aliagiza Kamati ya Uongozi ya Bunge kufanya kikao cha dharura saa saba mchana ili kujadili hoja hizo za wabunge kabla ya kuliarifu Bunge kwa kile kilichoafikiwa.
Taarifa ya Oscar Mbuza via HabariLeo

Kutokana na hali hiyo, jana wabunge walipendekeza Bunge hilo kukubali
kujadili mwenendo wa serikali kwa kile walichoeleza kwamba hawaridhishwi
na uwajibikaji wake, huku wengine wakiomba
kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kujadili hoja mbalimbali.
kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kujadili hoja mbalimbali.
Masuala yaliyosimamiwa na wabunge leo ni suala la fedha za akaunti ya Escrow Tegeta, mauaji ya kutisha wilayani Kiteto mkoani Manyara na uwajibikaji wa serikali katika siku za hivi karibuni.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM) ndiye alikuwa wa kwanza kuomba Mwongozo wa Spika, akishinikiza Bunge likubali kuunda Kamati Teule ili kuchunguza na kujadili madai ya ufisadi unaodaiwa kufanywa kwenye akaunti ya Escrow akidai kuwa kuna njama kwa ripoti hiyo kutowasilishwa bungeni.
Serukamba alisema suala la IPTL ni suala kubwa na sasa limesababisha wahisani kugoma kutoa fedha za kusaidia utekelezaji wa bajeti, lakini serikali imekuwa ikipiga danadana kuwasilisha ripoti kuhusu kuwepo kwa ufisadi katika Akaunti ya Escrow Tegeta.
“Mheshimiwa Mwenyekitio (Mussa Azzan Zungu), suala hili si la mchezo, leo hii wahisani wamegoma kutupa fedha, miradi imesimama, watu wanakufa lakini ripoti hailetwi.
“Mimi nadhani sasa Bunge lichukue mamlaka yake ya Kibunge.Tuunde Kamati Teule tuchunguze hili suala na kulifanyia uamuzi.
“Nasema hivyo kwa sababu tusipoangalia ripoti hii haitawasilishwa bungeni hadi siku tutakapoondoka,”
alisema Serukamba.
Mbunge aliyefuatia kwa suala hilo alikuwa ni Mbunge wa Mkanyageni, Habibu Mohammed Mnyaa (CUF) aliyesema serikali sasa imeingilia mamlaka huru ya Bunge na hivyo ni lazima Bunge likatae hali hiyo.
“Mheshimiwa Mwenyekiti ni lazima ifahamike kuwa Bunge ni mamlaka huru. Hii tabia ya Bunge kuanza kuingiliwa mamlaka yake haliwezi kuvumilika hata kidogo.
“Hili suala la IPTL lilianzia hapa bungeni na tuliambiwa uchunguzi utafanyika na ripoti italetwa bungeni ndani ya siku 45 lakini sasa ni mara mbili ya muda huo na serikali inaanza kuwakemea wabunge, jambo ambalo halikubaliki hata kidogo. Ni lazima sasa suala hili lipatiwe ufumbuzi,”
alisema Mnyaa.
Kwa upande wake Mbunge wa Ole, Rajabu Mbarouk Mohammed (CUF) alisema haridhishwi na uwajibikaji wa serikali katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa uhai wake na kulitaka Bunge likubali hoja yake ya wabunge kujadili mwenendo wa serikali.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama wabunge ni lazima sasa tusimame kama taasisi na
kujadili mwenendo wa hii serikali yetu. Mambo yanazidi kwenda vibaya, watu
wanauawa ovyo na hakuna hatua zinazochukuliwa.
“Leo hii Waziri anatoa tamko la serikali kuhusu mauaji ya Kiteto, lakini ukiangalia kwenye orodha ya shughuli za Bunge za leo, tamko hilo halipo.Lakini pia leo ni siku ya maswali kwa Waziri Mkuu, lakini hayupo na hakuna sababu tumeelezwa. Imefika mahala Waziri mmoja anajibu maswali
ya Wizara karibu nne, hii haikubaliki,”
alisema Mbunge huyo.
Naye Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (CHADEMA) alilitaka Bunge kujadili tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu mauaji ya Kiteto, akisema serikali imeshindwa kulipatia suala hilo ufumbuzi.
“Mheshimiwa Mwenyekiti tumesikia tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani kuhusu kinachotokea Kiteto. Lakini tamko lake linaonesha kasi ndogo sana ya kushughulikia na kukomesha mauaji haya.Kwa hali hiyo naliomba Bunge likubali tujadili suala hili ili tuweze kulipatia ufumbuzi,”
alisema Silinde.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Bunge Zungu aliposikiliza hoja hizo za wabunge alisema ni hoja nzito na zimefikia pabaya na aliagiza Kamati ya Uongozi ya Bunge kufanya kikao cha dharura saa saba mchana ili kujadili hoja hizo za wabunge kabla ya kuliarifu Bunge kwa kile kilichoafikiwa.
Taarifa ya Oscar Mbuza via HabariLeo
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment