Thursday, November 13, 2014

Roboti hiyo imetua kwenye kimondo daada ya safari ya miaka kumi angani 

Baada ya safari ya miaka kumi katika anga za juu, chombo cha anga za mbali cha Ulaya kimevuka kilomita chache za mwisho kutoka ardhini kutekeleza kile kitakachokuwa kifaa cha kwanza kuwahi kutengenezwa na binadamu kutua kwenye kimondo.


Roboti hiyo iliyotengezwa Ulaya kwa jina Philae, imefanikiwa kutua katika kimondo likiwa ni jambo la kihistoria kuwahi kushuhudiwa.

Aidha roboti hiyo ilitua katika Kimondo kinachojulikana kama 67P/Churyumov-Gerasimenko saa kumi jioni saa za Ulaya.

Kulikuwa na vifijo na nderemo pamoja na wanasayansi kupigana pambaja katika chumba ambako shughuli hiyo ilikuwa inadhibitiwa mjini Darmtadt, Ujerumani baada ya ishara kuonyesha kuwa roboti hiyo ilikuwa imetua kwenye kimondo. 

Ishara ya kuonyesha kuwa roboti hiyo ilifanikiwa kutua ulikuwa mwanga kutoka kwenye roboti hiyo. 

"Hii ni hatua kubwa sana katika historia ya binadamu kulingana na wanasayansi hao.

posted by bbc

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!