Friday, November 7, 2014

RAIA 13 wa Iran wamekamatwa wakiingiza nchini dawa za kulevya aina ya heroin zaidi ya kilogramu 41 yenye thamani ya shilingi bilioni mbili.

Wairani hao wamepandishwa kizimbani Jumatano Oktoba 5, 2014 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma ya kuingiza nchini dawa hizo za kulevya aina ya Heroin zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 2.


Walisomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Helen Moshi, mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda na kusomewa mashitaka na wakili wa serikali Hellen Moshi.

Washitakiwa hao Mansour Rais, Kheri Mohamed, Rasul Barh, Gulam Rezar, Nawab Bari, Said Muhamad, Nazir Pack, Mohamed Rafiq, Rahim Baksh, Salim Kosal , Yari Muhamad, Razar Rais na Allan Nuru, ambao ni wavuvi.

Wakili Hellen alidai washatakiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo Oktoba, 30 mwaka huu katika ukanda wa maji wa Tanzania jijini Dar es Salaam.

Alidai watuhumiwa hao walikutwa wakiingiza nchini gramu 41,713.57 za dawa za kulevya aina ya Heroin za thamani ya Sh.2,085,678,500 kinyume cha sheria.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, hakimu aliwataka washitakiwa wasijibu lolote kwakuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusilikiza kesi hiyo na kwamba upelelezi utakapokamilika itapelekwa Mahakama Kuu.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 18 mwaka huu itakapotajwa tena, na washitakiwa wamerudishwa rumande.

Wakati huohuo,raia watatu wa Nigeria na raia mmoja wa Iran wamepandishwa kizimbani mahakamani hapo kujibu shitaka la kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya Heroin za thamani ya zaidi ya Sh.bilioni 1.

Mbele ya Hakimu Emilius Mchauru, wakili wa serikali Janeth Kitali alidai,washitakiwa hao Chuks Agbazou, Ekoh Okafor, Emeka Nwachukwu na Waayat Khan, walitenda kosa hilo Oktoba 31 ,mwaka huu eneo la Tegeta Ununio, jijiniDar es Salaam.

Ilidaiwa kwamba washitakiwa walikutwa wakiingiza nchini gramu 35,208.66 za Heroin za thamani ya Sh. Bilioni 1.76 kinyume cha sheria.

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote ambapo upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 19 mwaka huu itakapotajwa.

  • FikraPevu: Wavuvi wa Iran waingiza dawa za kulevya nchini kwa meli za uvuvi

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!