Rais Shein
amefanya uteuzi huo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55 (1) cha
Katiba ya Zanzibar ya 1984.
Mhe. Said
Hassan Said ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na uteuzi huo
umeaza rasmi leo 7, Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Said Hassan
Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu.
Uteuzi wa
Mhe. Othman Masoud Othman umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1)
na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya
Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.
posted by paparazi
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment