Sunday, July 27, 2014


Kamishna wa jeshi Polisi katika mji wa Kwara nchini Nigeria Mr Ambrose Aisabor,amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa wawili miongoni mwa wengine, waliokuwa wakijishughulisha na uuzaji wa viungo vya binadamu.

Akihojiwa na waandishi wa habari kamishna Ambrose alisema watuhumiwa Amos Kareem na Abubakar Ladan,walikamatwa kufuatia msako mkali ulio endeshwa na jeshi hilo na baada ya kuhojiwa kwa masaa kadhaa watuhumiwa walikiri kuhusika na tukio hilo.

Aidha kamishna Ambrose amesisitiza kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa wengine.

Mmoja wa watuhumiwa, Abubakar Ladan, aliuambia mtandao wa Vanguard kwamba alikuwa ameahidiwa kupewa pikipiki kama angeweza kumpataia mteja wake kichwa, mkono na mguu wa binadamu.

Kwa mujibu wa mtuhumiwa , alidai kuwa nia ya yeye kufanya hivyo ni kutimiza ndoto yake ya kumiliki pikipiki hicho ndio kitu kilicho msukuma aende makaburini kufukua maiti na kukata kichwa,mguu na mkono kama inavyo onekana kwenye picha.

Mtuhumiwa wapili ambae ni Amos Kareem wakati akihojiwa alisema kuwa wateja wakubwa wa viungo hivyo ni wanasiasa na amesha wauzia mara nyingi,mtuhumiwa huyo alikataa kata kata kuwataja wanasiasa hao kwa majina kwa sababu za kiusalama dhidi yao.

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!