Sunday, July 27, 2014




Mfanyakazi wa ndani wa mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini Ciril Chami (CCM) aitwaye Mariam Said (16) amefariki dunia mapema alfajiri ya jana ikiaminika kwamba kifo chake kimesababishwa na kipigo toka kwa mke wa Mbunge Chami.



Sababu kubwa imeelezwa kuwa binti huyo ambaye ni muislamu alikataa kata kata kwenda kuhudhuria misa kanisani. Msimamo wa binti huyo ulimpelekea kipigo kikali, na hata mashuhuda walioshuhudia kipigo hicho cha kikatili kwa huyo binti.

Mke wa Mbunge inasemekana aliwajibu mashuhuda kwa lugha ya kejeli na kuwaambia hakuna mtu anaweza kumfanya chochote hata akimwua, kwani serikali 

ni yao, na CCM ndiyo inayoongoza dola, kwamba mahakama yetu, polisi wa kwetu, hakuna kima atakayenigusa. Alifoka mke wa Chami.
POSTED BY PAPARAZI>>>

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!