Kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambogo wilayani Rorya mkoani Mara, ambaye anadaiwa kupotea nyumbani kwa imani za kishirikina hatimaye amepatikana huku akiwa katika hali ya kutisha bila kujitambua na mwili wake ukiwa umejaa tope jingi, tukio ambalo limevuta mamia ya wananchi wa kijiji hicho.
Kijana huyo Kenedy oguko mwenye umri wa miaka 22
amekutwa nje ya nyumba yao asubuhi ya Juni 5 mwaka huu akiwa uchi wa
mnyama,ambapo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa
tangu kutoweka kwa kijana huyo siku nne zilizopita,wamekuwa wakimtafuta
bila mafanikio huku wakihusisha tukio hilo na imani za
kishirikina.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Rorya Bw Samwel Kiboye,ambaye ni miongoni mwa mashuhuda wa tukio
hilo amewaomba wananchi kuacha kulipiza visasi kwa kuwasaka watu
wanaotuhumiwa kwa ushirikina bali watumie vyombo vya dola huku
mwenyekiti wa kijiji hicho akilaani vikali vitendo hivyo vya ushirikina
vinavyoendelea kijijini hapo hatua ambayo amesema imesabisha wananchi
sasa kuishi kwa hofu kubwa.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza wazee wa jadi
kijijini hapo waliagiza kila mwananchi kupita mbele ya kijana huyo na
kumpa mkono kama njia moja wapo ya kuwezesha kupata fahamu kitendo
ambacho hata hivyo hakikuzaa matunda.
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment