Kuhusiana
na hizi picha 2 zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuznia asubuhi ya
leo, zikimuonyesha Mheshimiwa Mbunge huyo wa CCM Kapteni John Komba
akiwa kwenye mahaba na Mwanadada mmoja anayeishi Kinondoni. Mbunge huyo
amesema kwamba picha hizi zimetengenezwa na maadui wake wa kisiasa na
kwamba yeye sio Kiongozi wa hovyo hovyo namna hiyo. Kapteni Komba
amesema kwamba anawakaribisha wataalamu wa Picha na Mitandao
kutihibitisha ukweli wa picha hizo zinazoonyesha Mwana-Dada akiwa na
kipande cha khanga tu huku Mbunge huyo akiwa pembeni yake akionyesha
kutokuwepo kabisa kwenye Mahaba yanayotakiwa kuwa yanaendelea baina yao.
Mbunge huyo ameuliza zaidi iweje awe kwenye mapenzi kama picha zinavyo
onyesha halafu awe na nguo zake zote huku msichana akiwa na khanga tu?
Kapteni Komba amesema kwamba kama kweli Taifa hili limefikia hapa pa
kuchafuana namna hii kisa mitizamo tofauti ya kisiasa ya namna ya
kuongoza Taifa letu basi kama Taifa tumefikia pabaya sana. Mbunge huyo
amemalizia kwa kusema kwamba wale wote wanaomuamini kama Kiongozi
shupavu wa Taifa, wasikatishwe tamaa na wajinga wachache wenye mawazo ya
kitumwa ambao wanadhani wanaweza kummaliza kisiasa kwa kumtengenezea picha chafu kama hizi picha 2 za leo!! - Kapt. John Komba Mbunge wa Mbinga.
Friday, June 6, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment