Friday, May 16, 2014




Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliohusika na utekaji na unyan'ganyi wa gari Mei 12 mwaka huu eneo la Mlima Msangamwelu Wilaya ya Mbeya Vijini wameuawa na wananchi katika mapambano makali pembezoni mwa Mlima Mbeya.

Jambazi la kwanza lilitambuliwa kwa jina la Kitwana Lugoya(30)mkazi wa Ilemi Juhudi Jijini Mbeya ambaye aliuawa na wananchi baada ya kupata taarifa ambapo walifanikwa kumzingira na kufanikiwa kumkamata eneo la Msangamwelu Kata ya Mshewe.

Juhudi za wananchi ziliendelea kwa kushirikiana na Jeshi la kuwasaka majambazi wengine ziliendelea na kufanikiwa kuwakamata majambazi wengine wawili waliotambuliwa kwa majina ya Ndayobi Lutego(26)mkazi wa Igunga mkoani Tabora na Idd Sadiki(29) mkazi wa Veta Jijini Mbeya.

Hata hivyo juhudi za wananchi ziliendelea kuwasaka majambazi wengine wawili waliosalia wakiwa na bunduki na risasi kadhaa ambao walitokomea katika msitu mnene kupandisha Mlima Mbeya na kufanikiwa kukamata jambazi jingine lililokuwa na silaha na mfuko wa risasi ambapo wananchi walilidhibiti ndipo alirusha silaha na risasi msituni na kuanza kupambana na wananchi kwa kusaidiana na Askari na kufanikiwa kumkamata na katika mapambano hayo jambazi hilo liliuawa kwa kutumia silaha za jadi na mawe.






 Jambazi mwingine alikamatiwa katika Kitongoji cha Lunji Kijiji cha Ihombe kwa ushirikiano na wananchi wa vijiji vya Ihombe,Iziwa,Ikukwa na Msangamwelu ambalo pia lilipambana na wananchi hao na Askari majira ya saa tano asubuhi Mei 13 mwaka huu ambapo lildhibitiwa na kuuawa.

Mapambano hayo ya hatari katika msitu huo yalikuwa yakifanyika kwa tahadhari kubwa kutokana na kutojua idadi yao na aina ya silaha walizo nazo na mpaka sasa silaha na risasi havijapatikana katika msitu huo.

Baadhi ya majambazi kabla ya kuuawa imedaiwa kujihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Njombe,Iringa na Morogoro ambapo walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu na Jeshi la Polisi.





 Jeshi la Polisi limewashukuru wananchi waliojitolea kupambana na majambazi hao kwa kutumia dhana ya Polisi Jamii na ulinzi shirikishi ambayo imeanza kuzaa matunda na kufanikiwa kukomesha vitendo vya uhalifu Mkoani Mbeya ili Mbeya iwe na amani muda wote.

Wakati wa uporaji majambazi hayo yapatayo matano yalipanga mawe barabarani eneo la Msangamwelu na kufanikiwa kupora pesa,simu na pikipiki aina ya SANYA yenye namba T 682 CHT ambayo baadaye waliitelekeza msituni walipokuwa wanafuatiliwa na wananchi.





Majambazi hao walimjeruhi Dereva wa roli hilo aliyefahamika kwa jina la Sephen Mgogo ambaye amelazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi na miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya ambapo wawili kati yao hawajatambuliwa.

Jeshi la Polisi waliondoka Kijiji cha Ihombe majira ya saa moja na nusu usiku baada kazi ngumu ya kubeba miili ya majambazi hao mwendo wa masaa matano kwa miguu kutoka uneo la mapambano.

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!