Kamishna kova leo alipoamua kuitoa hadharani picha ya mtuhumiwa huyo mbele ya wanahabari ili apatikane mara moja
RONALD S/O MOLLEL ambaye ni mtuhumiwa wa ujambazi katika mabenki mbalimbali hapa jijini dar es salaam
Zipo taarifa za kuaminika kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na kushiriki kikamilifu katika matukio mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuongoza vikundi vya majambazi vilivyowahi kupora katika mabenki mbali mbali katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Mtuhumiwa huyo ni hatari kwani ana mtandao na watumishi muhimu katika matawi mbali mbali ya mabenki kwa lengo la kufanikisha uhalifu katika mabenki hayo.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa muhimu
ambaye ni kinara wa mtandao wa wizi katika mabenki ambaye anajulikana
kwa jina la RONALD S/O MOLLEL umri miaka 37, mfanyabishara na mkazi wa
Kimara Bonyokwa Jijini D’salaam.
Mtuhumiwa huyu amekimbilia mafichoni mara baada ya tukio la ujambazi
katika Tawi la Benki ya Barclays Kinondoni lililotokea tarehe 15/4/2014
ambapo majambazi walifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha
T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/= na EURO 2150/=. Aidha sasa
imefahamika kwamba mtuhumiwa huyu ni mume wa mtuhumiwa wa kwanza katika
tukio la Barclays Benki aitwaye ALUNE D/O KASILILIKA @ ALUNE D/O MOLLEL ,
miaka 28, Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa Benki Tawi la
Barclays Kinondoni. Mtuhumiwa Mollel anatafutwa kwa kila hali kwa vile
yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la Barclays na mara
baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo zilizoibiwa.RONALD S/O MOLLEL ambaye ni mtuhumiwa wa ujambazi katika mabenki mbalimbali hapa jijini dar es salaam
Zipo taarifa za kuaminika kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na kushiriki kikamilifu katika matukio mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuongoza vikundi vya majambazi vilivyowahi kupora katika mabenki mbali mbali katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Mtuhumiwa huyo ni hatari kwani ana mtandao na watumishi muhimu katika matawi mbali mbali ya mabenki kwa lengo la kufanikisha uhalifu katika mabenki hayo.
posted by PAPARAZI >>>
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment