Wednesday, May 28, 2014


Miili ya vijana hao ikiwa katika eneo la tukio muda mfupi baada ya kuchomwa moto

Watu wawili ambao hawajafahamika majina yao (20-25) wamefariki dunia kwa kupigwa na kisha kuchomwa moto katika kitongoji cha Iboja kijiji cha Mwime kata ya mwendakulima wilayani Kahama mkoani shinyanga. 









Tukio hilo limetokea leo majira ya saa nne asubuhi ambapo inadaiwa kuwa vijana hao wanatuhumiwa kwa kuiba Televisheni ya Mwananchi mmoja wa kijiji hicho. 



Mmoja wa Mashuhuda wa eneo hilo amesema aliona moshi baada ya kufika Shambani kwake ambapo aliamua kwenda kuangalia na kukuta miili ya watu hao ikiteketea kwa moto. 



Amesema aliujulisha uongozi wa kitongoji cha Iboja lakini haukufika na ndipo akatoa taarifa kwa jeshi la polisi wilaya ya Kahama, ambao wamefika katika eneo hilo na kuamuru uongozi wa kijiji cha Mwime kuzika miili hiyo.

Naye kaimu Afisa mtendaji wa kijiji hicho Paskal Lugembe amesema tayari wameanza juhudi za kuwakusanya wananchi ili washiriki katika shughuli ya kuwazika marehemu hao.

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!