MWANAMKE aliyejulikana kwa jina la Hadija Mohammed, mkazi wa Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam amekumbana na mkono wa sheria baada ya kufanya kitendo cha kinyama kufuatia kujifungulia kwenye ndoo kisha kichanga kukitupa chooni.
Kwa mujibu wa chanzo, mwanamke huyo alikuwa na ujauzito uliotimiza
miezi tisa na kila mtu alikuwa akiuona, lakini ghafla siku ya tukio
baadhi ya ndugu waligundua kuwa hakuwa na ujauzito tena!
NDUGU WAMBANA
Chanzo hicho kiliendelea
kutiririka kuwa baadhi ya ndugu na majirani walipomuona bila ujauzito
walimbana kwa kumuuliza iliko mimba hiyo.
“Ndugu zake na majirani walipomuona hana tumbo kama mwanzo
walishangaa, wakaamua kumbana tena kwa vitisho kwamba watampeleka
polisi.
“Ndipo alipoamua kueleza ukweli kwamba, alijifungulia kwenye ndoo lakini mtoto alikwenda kumtupa chooni,” kilisema chanzo hicho.
POLISI WAAMBIWA, WAKOMAA NAYE
Habari zilizidi
kudai kuwa baada ya majirani na ndugu kuambiwa hivyo walikwenda kutoa
taarifa kwenye Kituo cha Polisi Pangani kilichopo Ilala, Dar ambapo
walifika na kukiokoa kichanga hicho lakini walikuta kimeshakata roho.
MAMA APELEKWA POLISI
Mpashaji wetu alizidi kudai
kuwa, baada ya polisi kuuchukua mwili wa mtoto huyo hawakumwacha mama
mtu aendelee kuponda maisha uraiani, walimbeba mpaka kituoni hapo na
kumfungulia jalada lenye namba ILA/RB/1715/2014 kisha kumpeleka kwenye
Mahabusu ya Polisi Msimbazi huku mwili wa mtoto huyo ukipelekwa
Hospitali ya Amana na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
NI FUNDISHO
Afande mmoja ambaye aliomba jina
lake lisiandikwe, alisema ni lazima Hadija apambane na mkono wa sheria
ili iwe fundisho kwa wanawake wengine wenye mchezo huo.
“Hii tabia imekua sana. Wanawake wengi wanajifungua kisha wanawatupa
watoto chooni au kokote kusikojulikana ili wao waendelee kula raha
mjini. Huyu lazima sheria ishike makali yake ili iwe fundisho,” alisema
afande huyo.
posted by paparazi >>>
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment