Kiongozi
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema ni vyama
vitatu pekee vya upinzani ndivyo atakavyoviingiza kuunda baraza jipya la
mawaziri kivuli.
Mbowe
alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na NIPASHE lililotaka kujua muda
wa kuunda baraza hilo na idadi ya vyama atakavyoviingiza baada ya
kulivunja baraza la sasa wiki hii.
Alivitaja vyama hivyo kuwa ni Chadema, NCCR-Mageuzi na Chama cha Wananchi (CUF).
Kwa
mujibu wa Mbowe, sababu kubwa ya kuviingiza vyama hivyo kwenye baraza
hilo ni kutokana na msimamo wao wa kushiriki vyema katika mchakato wa
kupatikana kwa katiba mpya na kujadili Rasimu ya Katiba sura ya kwanza
na ya sita ya kwenye Mkutano wa Bunge Maalum la Katiba ulioahirishwa
Aprili 25, mwaka huu hadi ngwe ya pili kuanzia Agosti 5, mwaka huu.
“Ni vyama vitatu tu ambavyo vipo kikamilifu katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), yaani Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi.
Mrema (Augustine- TLP) yupo CCM na Cheyo (John-UDP) yupo nusu nusu, hivyo ni vyama hivyo vitatu tu ambavyo vipo Ukawa ndivyo vitakavyounda hili baraza jipya la mawaziri kivuli,” alifafanua Mbowe.
Mrema (Augustine- TLP) yupo CCM na Cheyo (John-UDP) yupo nusu nusu, hivyo ni vyama hivyo vitatu tu ambavyo vipo Ukawa ndivyo vitakavyounda hili baraza jipya la mawaziri kivuli,” alifafanua Mbowe.
Kuhusu
muda wa kuunda baraza hilo, Mbowe, alisema, yeye ndiye mwenye kuliunda
na kwamba baada ya kulivunja la sasa, atatangaza wakati wa kupatikana
kwa baraza jipya kwa kuwa la sasa bado lipo.
Kabla
ya Mbowe ambaye ni mjumbe wa Bunge la Katiba na Mbunge wa Jimbo la Hai
kutangaza maamuzi ya kufanya mabadiliko hayo, awali baraza hilo lilikuwa
likiundwa na wabunge wa Chadema pekee. Baraza hilo liliundwa mwaka 2011
baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuwashirikisha Chadema peke
yao.
Mbowe
alipounda baraza hilo alisema kuwa asingevihusisha vyama vingine vya
upinzani kwa kuwa wakati huo havikuwa na mwafaka wala maslahi
yanayofanana.
Hata
hivyo, aliahidi kuwa angewateua wabunge wa vyama vingine baada ya
kuridhika kwamba kambi ya upinzani ina mwafaka na msimamo wa pamoja
katika masuala mbalimbali muhimu kwa nchi.
Mbowe
alitangaza uamuzi wa kuundwa baraza jipya kivuli litakalovishirikisha
vyama vingine Aprili 30, mwaka huu baada ya yeye pamoja na wajumbe
wenzake wanaounda Ukawa, kufanya mkutano wa pamoja kwa lengo la
kusisitiza msimamo wa muundo wa serikali tatu na kupinga wa serikali
mbili unaoungwa mkono na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Viongozi
wote wa kitaifa wa vyama hivyo vinavyounda Ukawa walihudhuria Mbowe
alisema katika mkutano huo kuwa kulivunja baraza la sasa la mawaziri
kivuli ili kuwaingiza pia wajumbe kutoka vyama vingine vya upinzani na
kwamba ushirika uliopo baina vyama vyao hivyo hautaishia tu katika kudai
katiba ya wananchi, bali utaendelea hadi katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kutokana
na hilo, Mbowe, aliongeza kuwa wiki hii anatarajia kuvunja baraza la
mawaziri kivuli na kuliunda upya ili kuhakikisha Ukawa inasambaa siyo
katika Bunge Maalum la Katiba tu, bali katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na katika Uchaguzi Mkuu mwakani.
MREMA AZUNGUMZA
Alipoulizwa
jana na NIPASHE kuhusiana na kauli ya Mbowe, Mrema alihoji kwamba
wanaposema yeye ni CCM kwa nini hawazungumzii ndoa ya CCM na CUF ambao
waliunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
“Mbona
hiyo ndoa hawaisemi, badala yake wananisema mimi. Upinzani wa kusaliti
nchi, sitaufanya na yale ya kubomoa nchi sitayakubali,” alisema.
“Nimewahi
kushika Uwaziri wa Mambo ya Ndani, Kazi na Vijana pamoja na unaibu
Waziri Mkuu hivyo kuwa waziri kivuli ni maigizo,” alisema Mrema.
Mrema
pia alihoji ni kwanini baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanamuita
kuwa ni CCM wakati wao wanapoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni
Mwenyekiti wa CCM hawakatai uteuzi huo.
Cheyo alipotafutwa jana simu yake ilikuwa inaita bila majibu.
Mrema ni Mbunge pekee anayetoka Tanzania Labour (TLP) na Cheyo ni Mbunge pekee kutoka United Democratic (UDP).
posted by nipashe...
posted by nipashe...




0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment