FUNDI majengo Liu Fenghe wa nchini China, amenusurika kifo baada ya
kuchomwa na nondo kichwani na kuzama inchi 8 ambazo ni sawa na sentimita
20.
Liu alikuwa akiongea na rafiki yake na kwa bahati mbaya alidondokewa na nondo iliyomchoma kichwani.
Rafiki yake Liu aitwaye Zhang anasema:
"Ilikuwa ghafla. Kabla sijafanya chochote Liu alikuwa katika dimbwi la
damu."Inadhaniwa kuwa chuma hicho kilidondoka kutoka ghorofa ya 25 ya
jengo walilokuwemo mafundi hao mpaka kusababisha maafa hayo.
Picha ya X-ray ikionyesha jinsi nondo hiyo ilivyoingia kichwani mwa bwana Liu.
Madaktari walimfanyia upasuaji wa haraka katika hospitali iliyopo jimbo
la Shanghe nchini China na kueleza kuwa Liu hayupo tena katika hatari
japo bado haijajulikana ni lini ataweza kurudi kazini.
posted by paparazi






0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment