Thursday, November 26, 2015

Mahakama kuu kanda ya Mwanza, kuanzia muda huu, itaanza kusoma hukumu dhidi ya kesi ya kuruhusu kukusanyika kwa ibada na kuaga mwili wa kamanda Mawazo, aliekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita.
Mwanza mvua inanyeshwa na watu wengi wameshajitokeza katika viwanja vya mahakama kuu Mwanza.

Mawakili wa upande wa mashitaka wamekwishaingia wakiongozwa na Wakili Msomi John Milya, Poul Kipeja na James Ole Millya (MB).

Mzazi wa marehemu Mawazo, Mchungaji Charles Lugiko, baadhi ya wabunge wa UKAWA wameishaingia na mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh.Mbowe.

Jaji nae anaeingia anaketi na muda wowote hukumu itaanza kusomwa. Kama kawaida askari wametanda kila kona za barabara za kuingia mahakama kuu kanda ya Mwanza.

Update:
Jiji Lameck Malacha anaendelea kusoma maelezo ya upande wa mashitaka..

Last Uptade:
Familia ya Kamanda Mawazo na CHADEMA wamepewa haki zote za kumuaga na kumzika marehemu. Hivyo wameshinda kesi ya msingi dhidi ya serikali.



chanzo by jamiiforums
Ni agizo lililotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi. Marufuku shirika, taasisi au Idara ya Serikali kuchapisha hizo kadi. Fedha zilizotengwa zitumike kupunguza madeni ya wizara, taasisi na idara. Anayetaka kuchapisha, ametakiwa afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe.
Chanzo: Taarifa ya Ikulu.

Friday, February 6, 2015

JOPO la wanasheria lililoundwa kutoa tafsiri ya sheria katika sakata la kufukuzwa kwa madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Halmashauri ya Ilemela, mkoani Mwanza, limekamilisha kazi yake. 

SERIKALI imeingilia kati manyanyaso wanayopata wafanyabiashara ndogo na mamalishe nchini, kwa kuamua kuunda kikosi cha kiofisi, kitakachohusisha wajasiriamali hao kwa lengo la kukubaliana juu ya maeneo na muda mwafaka wa kuendesha shughuli zao. 

Wakati Taifa likipita katika kupindi kigumu cha kupima uadilifu wa viongozi, wengine wakijiuzulu na kuendelea kulalamika, NIPASHE imefanikiwa kupata barua ya kujiuzulu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi, ikithihibitisha jinsi kiongozi huyo alivyo juu kwa viwango vya utiifu na uadilifu.

Tuesday, February 3, 2015

Mara nyingi huwa sio kitu kigeni kwa mtu ambaye ni mjasiriamli wakati mwingine kufanya maamuzi yasiyo sahihi, kukosea hapa na pale na hata wakati mwingine kufanya biashara na watu ambao sio sahihi ambao wanauwezo wa kukurudisha nyuma, hii huwa inatokea sana bila kujua.

Mtambo maalumu wa kisasa kutoka Kampuni ya Ethicon ya Marekani utakaokuwa ukitumika katika upasuaji wa kawaida na ule wa matobo.

SERIKALI ya Tanzania inafanya jitihada za kuhakikisha kuwa inaondoa usumbufu wa upatikanaji wa viza za Uingereza na nchi nyingine ili kupunguza changamoto zinazowakumba wananchi wakati wa kuomba viza hizo.

Thursday, January 22, 2015


Unaweza kustaajabu na namna ya kipekee isiyomithilika, mandhari yake hutoa taaswira ya rangi ya dhahabu kila jua linapozama, huku mvumo wa mawimbi ya maji yenye kuchanua, yakigonga ukingoni mwa bahari ya hindi katika bustani ya Forodhani.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!