JOPO
la wanasheria lililoundwa kutoa tafsiri ya sheria katika sakata la
kufukuzwa kwa madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) katika Halmashauri ya Ilemela, mkoani Mwanza, limekamilisha
kazi yake.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda, alisema jana bungeni kwamba juzi alisaini barua
kwenda Tamisemi akitoa uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo.
Pinda
alisema hayo wakati akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa
Ilemela, Highness Kiwia (Chadema) aliyesema ni miaka miwili imepita,
lakini amekuwa hapatiwi majibu yenye matumaini juu ya suala hilo.
Katika
sakata hilo ambalo madiwani walifukuzwa kwa kutohudhuria vikao vitatu
vya kawaida vya Baraza la Madiwani, Kiwia alitaka kufahamu mustakabali
wa kata za Kirumba, Nyamanoro na Ilemela mbazo zimekosa uwakilishi
kutokana na hatua hiyo ya kufukuzwa.
Pinda alisema tatizo limekuwa la kisheria zaidi kuliko walivyofikiria.“Tuliunda jopo kutoa tafsiri ya sheria na tumemaliza kazi. Juzi nilisaini barua kwenda Tamisemi nikitoa uamuzi wa mwisho,” alisema.
Akijibu
swali la nyongeza la Mbunge Kiwia aliyeomba wananchi wa kata husika
wahakikishiwe ni lini uamuzi utawafikia, Pinda alisema, alisaini uamuzi
huo akiwa Dar es Salaam na kuupeleka kwa Waziri wa Tamisemi.
Alisema anaamini taarifa haitachukua muda mrefu kutolewa Tamisemi kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
POSTED BY PAPARAZIHURU
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment