SERIKALI ya Tanzania inafanya jitihada za kuhakikisha kuwa inaondoa
usumbufu wa upatikanaji wa viza za Uingereza na nchi nyingine ili
kupunguza changamoto zinazowakumba wananchi wakati wa kuomba viza hizo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakati akijibu swali la mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi, Jaku Ayoub aliyetaka kujua kauli ya Serikali kwa wananchi wanaopata usumbufu wakati wa kuomba viza za Uingereza.
Alisema Wizara yake inaendelea kuzisihi nchi hizo kulegeza masharti yao ya viza kwa Watanzania ili wananchi wa Tanzania waendelee kufaidika na uhusiano mzuri uliopo.
Alitoa wito kwa wananchi wenye dhamira ya kwenda Uingereza kufanya maombi ya viza mapema ili kuepuka usumbufu unaojitokeza pale wanapohitaji kusafiri .
Alibainisha kuwa Ubalozi wa Uingereza nchini haujafungwa ingawa huduma za viza zinatolewa kupitia wakala ambapo utaratibu wa upatikanaji wake ni ndani ya siku 18.
“Napenda kulihakikishia Bunge lako tukufu kuwa, Serikali inaendelea kufanya jitihada kuhakikisha usumbufu wa upatikanaji wa viza za Uingereza na nchi nyingine unapungua kwa kiasi kikubwa” alisema Waziri Maalim.
Kuhusu mchango wa uamuzi wa Tanzania kuwa na Ubalozi nchini Uingereza, Naibu Waziri Maalim alisema uamuzi huo umesaidia kukuza uhusiano wa kidiplomasia na Uingereza.
“Uhusiano ambao umetuwezesha kushirikiana katika nyanja za Elimu, Biashara, Utalii na Uwekezaji.Wanafuzni wa Tanzania wamekuwa wakinufaika na ufadhili wa Serikali ya Uingereza katika mafunzo ya Elimu ya Juu hususani Shahada za Uzamili na Uzamivu” alisema.
Aliongeza kuwa Sera ya Mambo ya Nje ya Kidiplomasia na uchumi inaendelea kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini ikizingatiwa kuwa Uingereza ni mdau mkubwa katika kuchangia bajeti ya taifa kupitia misaada mbalimbali wanayoitoa kupitia umoja wa Ulaya.

- Lorietha Laurence, Maelezo/Dodoma
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment