(picha via WhatsApp)
Kuna lugha mbili zinazotumika: “watanzania” na “wazawa”. Hizi ni tofauti kabisa.
Kuna mtu kashadadia hoja ya “wazawa” na kusema kuwa duniani kote ndivyo ilivyo. Pengine hatujaingia zaidi katika historia ya “uzawa” hapa nchini, na kwingineko. Yapaswa turejee mjadala wa uraia katika baraza la sheria la Tanganyika mwaka 1960, ambako hoja ya “uzawa” ilikuwa ikitumika kudai haki ya uraia, na haki ya utawala kwa watu weusi tu. Nyerere aliipinga na kutishia kujiuzuru uwaziri mkuu. Hoja hiyo ilijitokeza tena wakati wa ubinafsishaji ambapo wazawa walidai kupendelewa. Mwalimu aliipinga kwa nguvu na kuiita “ukaburu” rejea hotuba yake Kilimanjaro Hotel, mwaka 1995.
Hoja hii ilipoibuliwa na akina Mengi wakati wa gesi, “mzawa” ni nani hasa? Katika “wazawa” Bakhresa, Manji na Rostam wamo? Katika kile kisa cha Kongamano la Udasa nilichokisimulia hapo awali, Muhongo alitaja watanzania 10 walioohodhi umiliki katika madini. Mengi alikuwa wa tatu. Wakati akitaja majina mawili ya mwanzo, japo ni Watanzania, majina yao yanaonyesha dhahiri kuwa wana asili ya Kiasia. Washiriki katika Ukumbi wa Nkrumah walikuwa wakipiga kelele “sio wazawa hao”!
Kwa hiyo watetezi wa uzawa kueni macho, na mseme waziwazi kinachotetewa ni nini? Dhana ya Uzawa imeshatafitiwa vya kutosha (rejea vitabu vya Mamdani 1. Citizen and Subject; 2. When Victims become Killers; 3. Define and Rule), na imeonekana kuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya kisiasa pale ambapo “wazawa” wanahisi kunyang’anywa haki zao na “wahamiaji”. Mfano wake ni mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Hilo mosi. Pili, tunaposema “Watanzania wamiliki” tunamaanisha nini hasa? Hapa kuna watetezi wa mabepari wa bongo (akina Mwapachu); watetezi wa umiliki wa dola kwa niaba ya Watanzania; na watetezi wa mchanyato (dola + binafsi). Tungejikita katika kujadili njia hizi na kuonyesha ni ipi yenye tija na manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.
Kwa vyovyote vile, hapa nchini hakuna tabaka la mabepari wenye mtaji (national bourgeosie) bali tuna tabaka la mawakala (compradorial bourgeosie). Uwekezaji mkubwa binafsi wa ndani utahitaji tulijenge tabaka hilo, kwa kulipatia upendeleo na kuliruhusu kupora pale inapowezekana. Tufumbie macho Escrow, EPA, Richmond, ukwepaji kodi n.k., na tuwahimize hao waporao kuwekeza fedha “zao” katika shughuli za uzalishaji. Ndivyo zilivyofanya nchi zote zilizojenga tabaka la mabepari wa ndani, zikiwemo Japan na Malaysia. Ndiyo maana ya upendeleo kwa “wazawa” hiyo!

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment