Sunday, December 7, 2014

Prof.Anna Tibaijuka na Mfanyibiashara Rugemarila wakisakata dansi ( ?kusherekea mgao wa fedha za escrow? )
  • Vigogo waliopata mgao ni lini Watajiuzulu?
  • Watanzania tunaomba haraka mkondo wa sheria ufanye kazi zake
  • Watanzania tunaomba sherehe za vigogo watuhumiwa zifikike mwisho

Ni mategemeo yetu Watanzania wengi kuwa vigogo waliohusika kwa namna moja au nyingine katika sakata la fedha za Tegeta Escrow Account kuwa wanajiuzulu nafasi zao na mkondo wa sheria uwashughulikie haraka kwani hakuna aliye juu ya sheria.

Vigogo hawa wazito wanahusika kupokea mgao wa fedha za wavujajasho wa nchi hii lazima washughulikiwe na vyombo vya dola ili wawe mfano kwa wengine kuwa mvunja sheria lazima mkondo wa sheria umshughulikie.

Kwa kuwa kila kitu kiko wazi katika sakata zima Tageta Escrow Account na wahusika wametajwa, basi hakuna haja ya kesho au keshokutwa, bali wao wenyewe watuhumiwa wangeachia ngazi kwa kujiuzulu ili kuonesha uzalendo wao kuwa wanaziheshimu sheria za nchi na Katiba ambayo ndiyo mama wa sheria zote.

Lingekuwa jambo la kiungwana sana kama wangejiuzulu wenyewe kabla ya kuenguliwa na mamlaka iliyowateua.

Baadhi ya vigogo hawa wapo Maprofesa, sasa hawa viongozi wetu Maprofesa ndiyo ingekuwa wa mwanzo kuonesha mfano wa kujiuzulu. Mfano Waziri wa Ardhi, Prof.Anna Tibaijuka. Yeye kakubali kwa namna moja kuwa kapokea mgao Tsh. bilioni 1.6 akidai kuwa ni za shule zake, wakati shule zenyewe kuna baadhi ya walimu kutoka nje ya nchi mabo wanalipwa mishaara kwa dola za Marekani!


Ni vema Waziri, Anna Tibaijuka akaonyesha mfano kwanza wa kujiuzulu.

Pia tungeshauri hati zao za kusafiria au pasipoti za vigogo hawa zichukuliwe na idara husika za usalama hadi pale itakapothibitika kuwa hawana hatia.

SHERA MSUMENO UKATE HUKU NA HUKU


 Sijui tena kama patakuwa na kuchekeana kama hivi

POSTED BY WAVUTI.COM

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!