wabunge wakiwa katika vikao bungeni
Wabunge wa Kenya wametofautiana
vikali bungeni na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia
mjadala kuhusu mswada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani
wanasema unakiuka uhuru wa wakenya.
Bunge lililazimika kuahirisha
vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu
usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa
kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani walipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
Seneta Johnston Muthama alijipata pabaya kwani long'i yake iliraruliwa katika mvutano bungeni humo
Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama,
alijaribu kuyaja mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini
wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada
huo wakisema 'bado mapambano.'
Spika wa bunge Justin Muturi wakati
mmoja aliamuru walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika
bungeni humo kwa mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw
aupande wa upinzani.
Mswada huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia
matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza
kuwa washukiwaw augaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi
wakifanya uchunguzi.
Wabunge wakipitisha vipengee vya mswada huo vilivyofanyiwa marekebisho
Mapendekezo ya mswada huo ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali.
Pia
ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa
faini ya hadili shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha
ambazo zinaleta hofu na kusababisha taharuki.
Mswada huu umetolewa
kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Al Shabaab
wakilalamika na kutaka wanajeshi wa Kenya kuondolewa Somalia
Rais
Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo kuimarisha usalama wa tangui
mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari
la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.
POSTED BY BBC
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment