Prof. Tibajuka akizungumza katika ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam leo.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibajuka amekanusha taarifa zinasosambaa kuwa "ameachia ngazi" na kusema hawezi kujiuzulu Uwaziri kutokana kashfa ya fedha za akaunti ya Tegeta Escrow.
Akizungumza katika ukumbi wa Hoteli ya Hayyat Regency, Dar es Salaam, Prof. Tibaijuka alisema kuwa udalali wake fedha hiyo ni kwa ajili ya wanafunzi katika shule za Taasisi ya Johansson Girls Education Trust.
Alisema fedha hizo aliyoipata ni bilioni 1.66/= ambazo zilitoka katika kampuni ya James Rugemalira ni kwa ajili ya msaada wa shule za Taasisi ya Johansson Girls Education Trust.
Alisema kuwa fedha hiyo kuingia katika akauti yake binafsi ilitokana na masharti ya mtoa msaada ndugu James Rugemalira ambaye alitaka fedha hiyo iingie katika akauti ya Benki ya Mkombozi.
Alisema kuwa udalali wake ni kutafuta fedha kwa ajili ya elimu nchini ambapo, alidai hata Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi alitoa sh. milioni 248/= kwa ajili ya msaada wa shule hiyo.
Anna alisema kuwa wananchi watambue kuwa yeye ni mstaafu wa Umoja wa Mataifa hivyo kama angeitaka fedha hiyo angeweza kuifuata huko shuleni na kuchukua.




0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment