Monday, November 10, 2014

Kiongozi wa shirika la maendeloe la wanaume Kenya Nderitu Njoka (kushoto) na wanaume wenzake

Wanaume nchini Kenya wameelezea hisia mseto kuhusu wito wa kiongozi wa shirika la maendeleo la wanaume nchini humo kwamba hapo kesho tarehe 11 wasusie tendo la ndoa na kuonyesha hisia za mapenzi kwa wanawake.


Wiki jana kiongozi huyo Nderitu Njoka amewataka wanaume nchini Kenya kufanya hivyo kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru kwa wanaume inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 11 mwezi Novemba.

Bwana Nderitu amewataka wanaume wote kutojihusisha na wanawake kimwili , wawe wameoa au la kama ishara ya kuonyesha ghadhabu yao kwa ongezeko la dhuluma wanazotendewa wanaume pamoja na ongezeko la utumiaji wa dawa za kulevya na pombe miongoni mwa wanawake.

Wito huo hata hivyo umepuuzwa na baadhi ya wanaume ukitajwa kuwa njama ya bwana Nderitu kujipa umaarufu katika vyombo vya habari.

Hatua hiyo pia inatumiwa kjuonyesha kero la wanaume kutokana na hatua ya serikali kutenga shilingi bilioni mbili kwa mahitaji ya wasichana wakati ikikosa kutoa mchango kama huo katika kusadia wanaume wengi kufanyiwa tohara.

Njoka alinukuliwa akisema kuwa kidini wanaume ndio vipngozi wa familia lakini leo wamedhalilishwa huku wanawake wakitawala dunia.

POSTED BY BBC : Je wanaume watasusia ngono Kenya?

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!