Mazishi ya kitaifa yamefanyika
nchini Zambia kumuaga hayati Rais wa nchi hiyo Michael Sata aliyefariki
hospitalini mjini London Uingereza mwezi jana.
Sata alikuwa na
umri wa miaka 77 na maelfu ya watu walihudhuria mazishi hayo ambayo
yalikuwa kumbukumbu kwa maisha ya Sata pamoja na kilio cha kumpoteza
Rais huyo.Sata alichaguliwa mwaka 2011 baada ya miaka mingi ya kuwa katika upinzani na alisifika kwa jina la King Cobra kwa matamshi yake makali.
Katika wiki chache zilizopita, wanachi walitoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo ambaye mwili wake ulikuwa umelazwa katika majengo ya bunge.
Mazishi yalidhuriwa na viongozi mbali mbali wa kikanda.
Rais Sata alizikwa katika eneo lenye makaburi yaliyotengewa Marais wa nchi hiyo.
Taifa hilo kwa sasa linaongozwa na Rais wa muda huku uchaguzi mkuu ukipangwa kufanyika katika muda wa miezi michache ijayo.
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment