Rashid Makwiro a.k.a Chidi Benz
ambaye ameachiliwa kwa dhamana Jumatano wiki hii, amesimulia jinsi
ilivyokuwa hadi kukamatwa Ijumaa iliyopita Oct.24 na dawa za kulevya
kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere.
Chidi alizungumza na paparazi jana.
“Sikuwaambia natumia, niliwaambia dawa ambazo nilikuwa niko nazo lazima nitakuwa nimeconfuse kipindi ambacho natumia nilikuwa ofcoz naweka weka naficha ficha kwenye nguo nguo zangu na nini, so nimewambia maybe kwasababu hiyo nguo sijawahi vaa ndio mara ya kwanza…huwa naweka mashati kadhaa nayatundika tu hivi yako kama kumi kumi na tano, huwa nikivaa najua hili nasafiri nalo au nazunguka tu leo round za town baadae nikilivua nalitupa tu si unajua sisi mara nyingi nguo ukivaa unakuwa unavaa mara moja labda hivyo. So nahisi lazima ile dawa nilikuwa nimeiweka labda niliiweka au nimeficha coz nilikuwa naweza nikachukua hivi enzi zile sitaki mtu aone na nini naiweka kwenye mfuko naiacha hapo na hilo shati sijawahi vaa ndo nimelivaa juzi. “ alisema Chidi Benz.
“Shetta alinipigia simu akaniambia tunaondoka leo nikamwambia ooh yeah? Ooh yeah leo fasta, na mimi sasa hivi nakaa Tegeta unajua, so nikachukua lile shati fasta sio la kupiga pasi ni kama hili nililovaa hapa nikalichukua tu nikalipiga na jeans hivyo. Nikaenda zangu airport, niko airport nikamwambia Shetta namtania tu hivyo namwambia mdogo wangu nimebeba mambo nimebeba mambo [kicheko], nimebeba mambo kibao yale mabegi yamejaa yote haya yote mabegi sina nguo wala viatu wala nini hapa nina mambo tu like namtania unajua, lakini sasa nafika pale nasachiwa ndo nakutana na hiyo dawa”.
Aliendelea,
“Imagine nimekutwa na dawa kwenye mfuko wa shati kushoto unajua si kama nimeficha au nimefanya nini. Of course kila mtu anaongea cha kwake hamna yule muongo atakuwa hivi hamna mteja yule of course, so saivi lazima nikubali kwa kila mtu anachokiongea as long kwamba watu walikuwa hawasaidii chochote time ambayo sijakamatwa au sijakutwa hamna kitu chochote walikuwa mtu nasaidiwa au naambiwa kwahiyo naona kawaida tu.
Lakini si kitu nimepanga si kitu nilikuwa nimeplan unajua nimekutwa nayo mimi mwenyewe ndio nimejisachi, si yeye sijakamatwa mimi mwenyewe nimejisachi nimezitoa kushoto kulikuwa na pesa kulia pesa kushoto pesa tena akaniambia we pesa pesa akaniambia hapa mfukoni juu kuna nini, nikamwambia hii I think ni uchafu uchafu tu natoa hivi nakuta vidude kama kadhaa hivi naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona akaniambia bwana hii nini nikamwambia hii…dawa but sijui imekuaje na mimi pale kidogo kibinaadam nilikuwa kama kidogo akili imeniruka kuja kugundua kwamba ile ni dawa na nimeitoa mwenyewe unajua…
Yaani kwanza nakwambia kwasababu hata yeye wakati natoa hizo pesa nilikuwa kama namtania yule jamaa ananiambia mfuko wa nyuma namwambia hizi pesa huku pesa, hii karatasi yangu ya mashairi nataka niandike, hii huku pesa akaniambia na hapa juu nikamwambia hapo juu hamna kitu ni uchafu uchafu tu, hee natoa hivi nakutana na kimkanda unajua so like kama nilipigwa na butwaa hivi unajua.”
Chidi alisema alijaribu kuwaomba wana usalama wamuelewe na kumsamehe lakini ilishindikana.
“Nikajaribu kuwaomba jamaa nikawaambia bwana sorry kuna time nilikuwa natumia hizi vitu but nikaachana nazo, so wakati naachana nazo ofcoz zamani nilikuwa sio mtu wa kununua kimoja kimoja nilikuwa nanunua labda kadhaa unajua so navyohisi labda siku nilizichomeka kwenye kamfuko haka ka juu wa shati nikaziweka hapa nimesahau nguo nimeivaa tu ghafla nimesahau kiukweli, so please kama mnaweza kunielewa mkanisamehe please, hakuna ninachosafirisha hakuna nini mabegi yangu haya hapa mnaweza mkanisachi nisachini kote, wakasachi kila begi kila kitu hakuna kitu sina kitu kingine, nilikuwa na spika nilikuwa na viatu nilikuwa na nguo done.” alimaliza Chidi Benz
Kesi yake imepangwa kusikilizwa tena November 11.
POSTED BY PAPARAZIHURU
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment