JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma wa
Kituo cha Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la kumjeruhi mtumishi
wake wa ndani kwa mkumkata vidole vyake vinne vya mkono wa kulia kwa
panga, akimtuhumu kumwibia Deki ya Video nyumbani kwake.
JESHI LA POLISI LINASEMAJE?
Tukio hilo la kujeruhiwa kijana Steven Magessa (18), lilitokea Oktoba 20
mwaka huu katika kijiji cha Magange Mugumu wilayani Serengeti mkoani
Mara nyumbani kwao kijana huyo aliyekuwa amekimbilia huko baada ya
kudaiwa kumwibia mwajili wake nyumbani eneo la Igogo.
Akizungumza
na G.SENGO, kijana huyo alieleza kuwa kufanya kazi kwa askari huyo
kulikuja mara baada ya askari huyo kumfuata kijijini na
kuomba ridhaa ya wazazi wa kijana huyo kuambatana naye jijini Mwanza
ili kumsaidia kazi za nyumbani ambapo walikubaliana malipo ya kiasi cha
Sh 50,000/= kila mwezi jambo ambalo askari huyo alilikiuka na kushindwa
kulitekeleza kwa muda wa miezi sita.
“Nilipoona
hajanilipa mshahara wangu kwa muda wa miezi sita huku kila nikimwambia
ananijia juu na kunitukana matusi basi nilimuomba ruhusa ya
kwenda kijijini Oktoba 15 mwaka huu kumuona mama yangu mzazi aliyekuwa
anaumwa” alisema.
Steven alieleza kuwa wakati akiwa kijijini askari huyo (Mwajili wake)
alikuwa akimpigia simu kumtaka arudi Mwanza kuendelea na kazi na kudai
kuwa atamlipa malimbikizo ya mshahara wake kiasi cha Sh 300,000/=
zilizokuwa kama deni, Steven alikubali ombi hilo kwa kuomba atumiwe
nauli na pesa kidogo ya kumwachia mama yake, jambo ambalo askari huyo
alikaa kimya bila majibu.
“Siku ya Oktoba 20 mwaka huu majira ya saa 4:00 asubuhi alifika kijijini
akiwa na askari watatu kwenye gari la Polisi (Difenda) wa Kituo cha
Mugumu na kudai kuwa nipo chini ya ulinzi kisha kunifunga pingu, akidai
kuwa nilimwibia Deki ya Video na kutoroka nyumbani kwake, walinipandisha
kwenye Difenda kunipeleka kituoni “ alisema.
Kijana huyo alieleza kuwa baada ya kufikishwa kituoni Mugumu askari huyo
na wenzake walianza kumuhoji huku wakimpa maneno ya vitisho.
Kijana
huyo alipokataa kuwa hakuiba wala kutoroka, Sajenti Fatuma aliamuru
kijana huyo kuvulishwa shati alilovaa na kisha akafungwa usoni na
kuombwa anyooshe mkono mezani ili apewe 'Sapraizi'.
"Sekunde chache nilihisi kitu kikali kimenipitia kwenye vidole vyangu
vinne vya mkono wa kulia na kufuatiwa na maumivu makali, niliusogeza
mkono wangu mdomoni kuupoza kwa kuupuliza ndipo nilipo gundua kuwa
nimekatwa kabisa vidole vyangu vinne vya mkono wangu wa kulia ikibakia
dole gumba tu" kijana Steven alisimulia kwa uchungu.
“Niliangua
kilio kutokana na maumivu na sijui vidole vyangu hadi sasa vikowapi,
askari wenzake baada ya kuona nimetokwa na damu nyingi
walimshauri anipeleke hospitali ya Wilaya ya Mugumu ili nipatiwe
matibabu kabla ya kuondoka kuja Mwanza,” alisisitiza.
Steven alisema baada ya kupatiwa matibabu, tulienda kupanda basi ili
kuja Mwanza kwa madai kuwa amenifungulia kesi ya wizi wa Deki ya Video
na tuliopofika alinipeleka kituo cha Polisi Kati Nyamagana na kuniweka
Mahabusu akinituhumu wizi, lakini nilipochukuliwa maelezo nilikana
tuhuma za wizi na kueleza ukweli wangu ili kupata msaada.
Taarifa zingine kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa
askari huyo alikusudia kufanya ukatili huo kutokana na udanganyifu ambao
alifanya kwa uongozi wake akiomba kupatiwa silaha (SMG) kwa ajili ya
kuitumia kwenye kazi za nje lakini lengo ikiwa ni kwenda na silaha hiyo
kwa ajili ya kumkamata na kumtishia kijana huyo, jambo ambalo uongozi
ulimgomea.
JESHI LA POLISI LINASEMAJE?
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC), Valentino Mlowola, jana
ofisini kwake amethibitisha kuwepo kwa taarifa za tukio hilo na kueleza
kuwa tayari Jeshi hilo limechukuwa hatua madhubuti, hatua ya awali ikiwa
ni kumshikilia askari huyo kwa kufanya ukatili huo
na kujichukulia sheria mkononi kumjeruhi kijana huyo.
Mlowola alisema pamoja na kijana huyo awali kufunguliwa jalada la
kutuhumiwa kufanya kosa la wizi (Jinai) na kudaiwa kutorokea kijijini
kwao, bado askari huyo alitakiwa kufuata mfumo wa kiutawala na kisheria
uliopo kushughulikia suala hilo badala ya kuamua kujichukulia maamuzi ya
kumwadhibu mtuhumiwa kabla ya uthibitisho wa mashitaka yaliyokuwa
yamefungulia.
“Nilizipokea taarifa hizi kwa mshangao na masikitiko makubwa na
zimenisitua sana. Si kitendo cha kiungwana hata kidogo kwa mtu ambaye
anatakiwa kufuata taratibu za mfumo wa utawala na sheria katika
utekelezaji wa kushughulikia kero na matatizo ya jamii.
"Alitakiwa kutumia busara kwani tayari alishamfungulia jalada la kumtuhumu kumwibia ikizingatiwa naye ni mzazi wa watoto watano ni lazima anaujua uchungu,”alisema.
"Alitakiwa kutumia busara kwani tayari alishamfungulia jalada la kumtuhumu kumwibia ikizingatiwa naye ni mzazi wa watoto watano ni lazima anaujua uchungu,”alisema.
Kamanda Mlowola alisema kuwa, kufuatia ukatili huo kufanywa na askari wake,
ameunda timu ya kikosi cha askari kwenda kijijini Magange wilayani
Serengeti mkoani Mara ili kufanya uchunguzi wa tukio hili ikiwa ni
pamoja na kufanya mahojiano na familia, wananchi wa kijiji hicho kisha
Hospitali ya Wilaya ya Serengeti alipopatiwa matibabu ya awali.
“Ili tupate ukweli wa jambo hili tumeunda timu hiyo, kwani kijana Steven
tumemhoji ametueleza askari Fatuma alichomfanyia na kudai
hakumwibia. Lakini askri wetu pia amehojiwa, awali amedai hakufanya
kitendo hicho bali wananchi ndo walimfanyia ukatili huo hivyo ni
mkanganyiko lakini ukweli utapatikana tu ” alisisitiza.
Mlowola aliongeza: "Tayari tunamshikilia askari huyu na tumemfungulia
jalada la uchunguzi kwa taratibu za kijeshi na ikibainika katenda kosa
hilo tutamfukuza kazi na kumfikisha katika vyombo vya sheria ili
kuchukuliwa hatua zaidi kulingana na kosa alilofanya, lakini pia kijana
Steven naye anashikiliwa kwa tuhuma alizonazo za wizi kufuatia jalada
lililopo.
“Hatuwezi kuendelea kucheka na kufumbia macho kitendo hiki maana ni jambo
ambalo linamgusa kila mtu hata mimi ni mzazi ukiachana na utumishi wangu
wa umma. Ntahakikisha jambo hili nalishughulikia kwa umakini na kutoa
taarifa kwa umma ili pia kueleza wananchi kuwa tukio hili limefanywa na
mtumishi kama mtu si Taasisi ya Jeshi la Polisi .”
POSTED BY PAPARAZIHURU
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment