JESHI la Polisi Zanzibar, linawashikilia
watu saba kwa tuhuma za kutekeleza shambulizi la bomu katika maeneo ya
Darajani na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine saba kujeruhiwa.
Akizungumza na gazaeti hili ofisini
kwake Ziwani, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa jeshi
la polisi, DCI, Yussuf Ilembo ,alisema watuhumiwa hao walikamatwa Juni
18 mwaka huu majira ya usiku katika maeneo mbali mbali ya mi wa
Zanzibar.
Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya watuhumiwa hao akisema bado upelelezi unaendelea.
Alisema watuhumiwa wamepelekwa makao mkuu ya polisi Dar es Salaam kwa mahojiano.
Alisema watuhumiwa wamepelekwa makao mkuu ya polisi Dar es Salaam kwa mahojiano.
Aliwataka wananchi kuacha kufuata
vishwawishi na kurubuniwa na watu au makundi ya kihalifu kwa lengo la
kuchafua amani na kuwatia hofu wananchi.
Tukio hilo la bomu lilitokea wika Juni
13 majira ya saa 2:30 za usiku katika maeneo ya Darajani ya mjini Unguja
na kuwalenga wahubiri wa amani wa dini ya kiislamu waliokuwa nje ya
msikiti.
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni
Kassim Issa Muhammed (36) ,Hamad Nassor Kassim (46) , Khelef Abdalla
Abdalla (21), Khalid Ahmed Haidar (16) , Ahmed Haidar Jabir (47) na
Suleiman Ali Juma (21) huku marehemu akitambulika kwa jina la Mohammed
Khatib Mkombalaguha (26) mwenyeji wa Tanga.
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment