Mtuhumiwa
wa wizi wa ng'ombe akiwa kwenye majani yaliyotumika kumchochea moto
mara baada ya kupata mkong'oto wa nguvu kutoka kwa wamiliki wa ng'ombe
hao huko Mwasanga, Ivumwe jijini Mbeya.
MTU mmoja
anayetuhumiwa kwa wizi wa ng’ombe na ndama wake, mwishoni mwa wiki
iliyopita alipata kipigo cha kufa mtu na baadaye kuchomwa moto, lakini
katika hali isiyo ya kawaida, hakuweza kufariki ‘kugoma kufa’ hadi
polisi walipotokea na kunusuru maisha yake.tukio hilo lilitokea Mwasanga, Ivumwe jijini Mbeya kufuatia kuibiwa kwa wanyama hao usiku nyumbani kwa Kongoro Mwakitalima, ambaye ni mkazi wa Isyesye Kata ya Ilomba.
Ilidaiwa
baada ya mwizi huyo kuwachukua wanyama hao, mtu huyo aliwapa taarifa
majirani zake, ambao asubuhi na mapema walijihimu na kuanza kuwatafuta
ambapo baada ya kufika eneo la Ivumwe walikutana na mwendesha bodaboda
ambaye aliwaambia alikutana na mtu akiwa anaswaga mifugo hiyo.
Walipoambiwa
hivyo, wananchi hao wakitumia bodaboda, walimfukuzia mtu huyo na
kufanikiwa kumkuta katika eneo la Mwasanga relini akiwa na ng’ombe hao.
Shuhuda
alisema wananchi walikusanyika na kuanza kumshushia kipigo kikali,
lakini licha ya uzito wa mkong’oto, bado mtuhumiwa huyo alionekana kuwa
ngangari ndipo waliamua kumchoma moto.
Hata hivyo, licha ya moto huo, bado mtu huyo hakuweza kukata roho hadi askari polisi walipofika eneo hilo na kumchukua.
Hata hivyo, licha ya moto huo, bado mtu huyo hakuweza kukata roho hadi askari polisi walipofika eneo hilo na kumchukua.
Hadi tunaingia mtamboni hakuna taarifa zilizothibitisha kama mtuhumiwa huyo alikuwa hai au la!
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment